1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Paris. Wafaransa waliopotea wapatikana.

5 Machi 2007
https://p.dw.com/p/CCM7

Ufaransa imesema kuwa raia wake saba ambao walipotea nchini Ethiopia wamepatikana wakiwa wako salama.

Ni miongoni mwa kiasi cha wageni 20 na wasindikizaji wenyeji ambao walipotea wiki iliyopita wakati wakifanya ziara katika eneo la Afar, eneo ambalo waasi wanaotaka kujitenga wanafanya shughuli zao.

Maafisa wanatuhumu kuwa watu hao waliopotea, ambao ni pamoja na Waingereza watano, wametekwa nyara. Baadhi ya raia hao wa Uingereza ni wafanyakazi wa ubalozi wa nchi hiyo nchini Ethiopia.