1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

PARIS:Mshukiwa wa mauaji ya Rwanda achunguzwa

25 Oktoba 2007
https://p.dw.com/p/C7Co

Mahakama ya rufaa mjini Paris nchini Ufaransa inachunguza madai ya Mahakama ya Umoja wa mataifa ya uhalifu wa kivita ya kumrejesha nyumbani mshukiwa wa mauaji ya halaiki ya Rwanda.Mshukiwa huyo yuko nchini Ufaransa nayo mahakama ya uhalifu wa kivita inadai kurejeshwa kwake ifikapo Novemba tarehe saba.Mahakama hiyo ya Ufaransa aidha inatathmini uwezekano wa kumuachia Dominique Ntawukuriryayo anayesakwa kwa kuhusika na mauaji hayo ya mwaka 94.

Ntawukuriryayo alikamatwa wiki jana na polisi wa Ufaransa kwenye eneo la kusini la Ufaransa na anazuiliwa jela nchini humo kwa sasa.Mahakama ya ICTR inamsaka kwa kuhusika na mauaji ya halaiki ya Rwanda.Afisa huyo wa zamani ameishi nchini Ufaransa tangu mwaka 99 na ana hati za ukazi wa Ufaransa amekanusha madai hayo na akaeleza kutaka kesi yake kusikilizwa Ufaransa