1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

PARIS:Utafiti katika pembe za ncha ya dunia waanza

1 Machi 2007
https://p.dw.com/p/CCNS

Wanasayansi kutoka mataifa zaidi ya 60 wanaanza utafiti katika eneo la ncha za dunia za kaskazini na Kusini la Aktiki huku ulimwengu ukikabiliwa na changamoto ya athari za ongezeko la joto ulimwenguni.

Utafiti huo wa eneo la ncha za dunia katika mpango wa mwaka wa International Polar Year unalenga kutathmini vichafuzi vya mazingira,viumbe vya baharini mfano planktoni vilevile afya ya dubwi wa eneo hilo na pengwini yaani Penguin.

Wakati wa uzinduzi rasmi wa utafiti huo mjini Paris nchini Ufaransa,Mkuu wa Shirika la Utabiri wa hali ya anga ulimwenguni Michel Jarraud anasema kuwa maeneo ya ncha za dunia yako hatarini.Kulingana na wanasayansi kupungua kwa theluji kwenye bahari ya Aktiki vilevile mito ya barafu katika eneo hilo ni ishara kuwa viwango vya joto vinaongezeka.Utafiti wa aina hiyo ulifanyika mwisho mwaka ’57 na ’58.