1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

PARIS:Wafaransa kupiga kura hii leo katika uchaguzi wa rais wa marudio

6 Mei 2007
https://p.dw.com/p/CC4V

Wananchi wa Ufaransa leo wanapiga kura katika uchaguzi wa marudio wa urais nchini humo, ambapo wagombea wawili wanachuana vikali.

Nicolas Zakozy kutoka chama cha kihafidhina cha UMP na Bi Segolene Royal kutoka chama cha kisoshalisti wanaingia katika duru ya pili baada ya uchaguzi wa kwanza kushindwa kutoa mshindi.

Tayari hata hivyo kura zimechapigwa katika maeneo yaliyochini ya himaya ya Ufaransa, kama vile visiwa vya Saint Pieere na Maquelon ambavyo viko katika pwani ya Mashariki mwa Canada.

Pia visiwa vya Martinique na Guadalope vilivyoko Caribbian, wananchi wake walianza mapema kupiga kura.

Kura za maoni za hivi karibuni zinaonesha kuwa bwana Sakozy anaongoza kwa asilimia nane mbele ya Bi Royal.