1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

PARIS:Wagombea wawili wa urais washutumiana kwenye mjadala wa TV

3 Mei 2007
https://p.dw.com/p/CC5B

Zikisalia siku chache kuingia kwenye duru ya pili ya uchaguzi war ais nchini Ufaransa, wagombea wawili wa urais nchini humo wamekabiliana katika mjadala wa televisheni uliochukua muda wa saa 2.5.

Katika mjadala huo Segolene Royal wa chama cha kisosholisti amemshutumu mpinzani wake Nicolas Sarkozy kwa kuchangia kushindwa kwa Ufaransa kukabiliana na tatizo la ukosefu wa ajira na kuongezeka kwa visa vya uhalifu.

Kwa upande wake bwana Sarkozy amesema muda wa kufanya kazi wa saa 35 kwa wiki nchini humo ni janga kubwa kwa uchumi wa nchi hiyo.

Muda huo wa masaa ya kufanya kazi ulianzishwa na serikali ya mwisho ya kisosholisti.

Mjadala huo umetazamwa na kiasi nusu ya watu wazima nchini humo.

Mjaladala huo uliokuwa unasubiriwa kwa hamu ni muhimu katika matokeo ya uchaguzi wa jumapili.