1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

PASHAWAR:Sita wauawa katika shambulizi la kujitoa mhanga

4 Agosti 2007
https://p.dw.com/p/CBcF

Watu sita wameuawa na wengine 31 wamejeruhiwa baada ya mshambuliaji wa kujitoa mhanga kujilipua katika kituo cha basi kilichokuwa na watu wengi huko Kaskazini Magharibi mwa Pakistan.

Msemaji wa Polisi katika jimbo la Pashawar amesema kuwa mshambuliaji huyo alijilipua ndani ya gari alilokuwa akiendesha mara baada ya kufika kwenye kituo hicho cha basi kilichokuwa kimejaa watu.

Katika shambulizi lingine huko huko Pakistan, wanamgambo wanaoliunga mkono kundi la Taliban waliwafyatulia risasi na kuwaua askari wanne kwenye kituo cha ukaguzi katika jimbo la Waziristan.Polisi walifanikiwa nao kuwauawa wanamgambo kumi.