1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

PESHAWAR: Mripuko wa bomu umeua 25 Pakistan

15 Mei 2007
https://p.dw.com/p/CC1l

Hadi watu 25 wameuawa mjini Peshawar,kaskazini-magharibi ya Pakistan katika shambulio la bomu, ikidhaniwa kuwa limefanywa na mwanamgambo aliejitolea muhanga.Miongoni mwa wale waliouawa ni wanawake wawili na mtoto mmoja.Zaidi ya watu dazeni mbili pia walijeruhiwa katika mripuko huo wa bomu uliotokea kwenye ukumbi wa chakula katika hoteli inayomilikiwa na Muafghanistan.Mashahidi wamesema baadhi kubwa ya watu waliouawa au kujeruhiwa ni raia wa Afghanistan.Hakuna aliedai kuhusika na shambulizi hilo.Vile vile haijulikani ikiwa shambulio hilo linahusika na mapambano yaliyozuka mwishoni mwa juma kati ya wafuasi wa serikali na wanaharakati wa upinzani,katika mji wa Karachi,kusini mwa nchi.Watu 40 waliuawa katika machafuko hayo.