1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

PETRA: Mfalme Abdullah amekutana na Olmert

15 Mei 2007
https://p.dw.com/p/CC1p

Mflame Abdallah wa Pili wa Jordan amekutana na Waziri Mkuu wa Israel Ehud Olmert katika juhudi ya kutafuta suluhisho la amani.Olmert aliwasili mji wa kale wa Petra nchini Jordan kwa mkutano pekee wa ngazi ya juu pembezoni mwa mkutano unaofanywa na wapokea zawadi ya amani ya Nobel pamoja na vijana wa Kiisraeli na Kiarabu wakitafuta njia za kusuluhisha migogoro ya Mashariki ya Kati.Jordan na Misri ni nchi za Kiarabu za kwanza kutia saini mikataba ya amani pamoja na Israel.Nchi hizo mbili zina dhima ya kuhimiza mpango wa amani uliopendekezwa na nchi za Kiarabu.