1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kamati yapendekeza Pistorius aondolewe gerezani

8 Juni 2015

Mwanariadha mlemavu wa Afrika Kusini Oscar Pistorius aliyepatikana na hatia ya kuumua mpenzi wake Reeva Steenkamp huenda akaachiliwa huru tarehe 21 Agosti:

https://p.dw.com/p/1Fdg4
Oscar Pistorius Urteil 21.10.2014
Picha: Reuters/S. Sibeko

Kwa mujibu wa taarifa za idara ya magereza ya Afrika Kusini mwanariadha huyo aliyekuwa amehukumiwa kifungo cha miaka mitano jela huenda akasamehewa.

Kaimu kamishna wa kitaifa wa magereza Zach Modise amesema leo kuwa kamati moja ya gereza ilipendekeza wiki iliyopita kuwa Pistorius aachiliwe huru kutoka gereza la Pretoria mnamo Agosti 21, ikiwa ni miaka 10 baada ya kuhukumiwa kifungo jela, maana kuwa amekitumikia kima cha chini cha kifungo chake kilichostahiki.

Modise amesema uamuzi huo umetokana na kuwa Pistorius ameonyesha tabia nzuri gerezani. Msemaji wa Magereza Manelisi Wolela amesema mazingira halisi ya Pistorius kupewa kifungo cha nyumbani hayatafichuliwa kwa umma.

Pistorius alifungwa mnamo Oktoba 21 mwaka uliopita katika kesi iliyovutia hisia kali kutoka kote duniani.

Mwandishi: Bruce Amani/AFP/DPA/AP/reuters
Mhariri: Yusuf Saumu