1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

PMaoni ya wahariri

Mtullya, Abdu Said26 Februari 2008

Wahariri wanatoa maoni juu ya kuunda miseto.

https://p.dw.com/p/DDSn
Magazeti ya UjerumaniPicha: picture-alliance/ dpa



Wakati umebakia mwaka mmoja na nusu  kabla ya uchaguzi mkuu kufanyika nchini Ujerumani vyama vya siasa vimo katika patashika ya kuunda miseto.

Wahariri wa magazeti wanatoa maoni yao juu ya patashika hizo.


Jee nani ashirikiane na nani katika kuunda serikali? Swali hilo lisingetokea thama na ujio wa nguvu wa chama cha mlengo wa kushoto-kwani chama cha Social demokratik kilichomo katika serikali ya  mseto  kinafikiria sana kushirikiana na chama hicho japo katika ngazi ya majimbo. Jambo hilo linaonekana kama kufuru kwa wengi nchini Ujerumani.

Lakini chama kingine kikuu, CDU kilichomo katika serikali ya mseto vilevile nacho kinafikiria kuunda mseto na chama cha kijani.

Gazeti la NORDBAYERISCHE KURIER linasema hakuna  ubaya ikiwa chama hicho cha CDU kitashirikiana na chama cha kijani katika jimbo la Hamburg.

Lakini Mhariri wagazeti hilo pia  anatilia maanani, ukweli kwamba  chama  cha mlengo wa kushoto cha wakomunisti wa zamani kimejijenga vizuri. Na kutokana na  hayo  mhariri wa gazeti la NORDBAYERISCHE anavitaka vyama vyote vifikirie upya.

Katika maoni yake gazeti la RHEIN- NECKER pia linasema, mseto baina ya CDU na chama cha kijani, litakuwa jambo la kuvutia katika  siasa za Ujerumani.

Gazeti  la HANDELSBLATT linakilaumu vikali chama cha Social Demokratik kwa kubadili nia juu ya chama cha mlengo wa kushoko -yaani chama cha wakomunisti wa zamani.

Gazeti linasema chama hicho kimo katika mkondo wa kujiharibia katika uchaguzi mkuu utakaofanyika mwezi septemba mwakani nchini Ujerumani.

Gazeti linasema msimamo wa sasa wa mwenyekiti wa chama cha Social Demokratik Kurt Beck utawafukuza wastahiki  ambao katika  mazingira mengine wangekipigia kura chama hicho. Na jambo baya zaidi, anasema mhariri ni  iwapo mjumbe wa chama cha SPD Andrea Ypsilanti atatumia msaada wa  kura za wakomunisti na wanaitikadi kali  wa mlengo wa kushoto ili kuwa waziri mkuu wa jimbo la Hesse.

Lakini gazeti la ESSLINGER linasema,hayo yatasahauliwa haraka na wananchi.

Mhariri wa gazeti hilo anasema yumkini wastahiki wamebaini kuwa mwenyekiti wa chama cha Social Demokratik bwana Beck amevunja neno lake, lakini hasira za  wapiga kura hao hazitadumu muda mrefu.

Gazeti linasema watu wamezoea kuwaona  wanasiasa wakivunja  ahadi zao.

Na kwa hakika watu hawajali ni chama gani kinashirikiana na nani. Muhimu kwao ni maudhui ya siasa.