1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Podolski hatacheza hadi mwisho wa mwaka

Josephat Nyiro Charo4 Septemba 2013

Ni pigo lengine kwa kocha wa timu ya taifa ya kandanda ya Ujerumani, Joachim Löw. Podolski hatacheza tena mwaka huu wa 2013. Bastian Schweinsteiger, Mario Götze na Ilkay Gundogan pia wameumia.

https://p.dw.com/p/19buT
epa03839535 Lukas Podolski of Arsenal reacts after receiving an injury during the UEFA Champions League qualification playoff second leg soccer match between Arsenal FC and Fenerbahce in London, Britain, 27 August 2013. EPA/KERIM OKTEN
Fußball Champions League Arsenal gegen Fenerbahce Istanbul Verletzung Lukas PodolskiiPicha: picture-alliance/dpa

Jeraha kwenye goti alilolipata mchezaji wa safu ya mashambulizi ya timu ya taifa ya Ujerumani, Lukas Podolski, ni baya zaidi kuliko ilivyohofiwa hapo awali. Hii ina maana mshambuliaji huyo wa klabu ya Arsenal London hatacheza hadi mwezi Desemba mwaka huu.

Daktari wa timu ya taifa ya kandanda ya Ujerumani, Hans-Wilhelm Mueller-Wohlfahrt, amemfanyia uchunguzi Podolski mjini Munich na kugundua amekatika ukano wa mvungu wa goti la mguu wake wa kushoto. "Kwa bahati mbaya sitaweza kucheza kwa muda mrefu, kama miezi mitatu," Podolski ameliambia gazeti la kila siku la Ujerumani, Bild.

Podolski atakosa mechi za kufuzu kwa kombe la dunia la kandanda nchini Brazil mwakani zilizosalia mwaka huu. Alitolewa uwanjani akiwa kwenye machela dakika ya 50 ya mechi kati ya klabu yake ya Arsenal na Fernerbahce Istanbul wiki iliyopita, wakati ilipofikiriwa angekuwa nje ya uwanja bila kucheza mechi yoyote kwa wiki hadi 10.

Mwandishi: Josephat Charo/APE

Mhariri: Iddi Sessanga