1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Poland yagoma kusaidia uchunguzi wa umoja wa Ulaya.

12 Novemba 2006

Wawakilishi wa tume ya bunge la Ulaya , wanaochunguza madai ya kuwapo kwa misafara ya ndege ya shirika la ujasusi la Marekani CIA katika bara la Ulaya , imeshutumu ushirikiano unaotolewa na serikali ya Polend baada ya kuitembelea nchi hiyo katika muda wa siku tatu. Taarifa ya Thomas Rautenberg inasomwa studioni na Sekione Kitojo.

https://p.dw.com/p/CHL9

Ujinga na dharau ndivyo walivyokumbana navyo tume ya bunge ya umoja wa Ulaya inayochunguza iwapo kulikuwa na uwezekano wa kuwapo jela za siri za CIA katika bara la Ulaya katika serikali ya Poland.

Carlos Coelho , mwenyekiti wa tume hiyo, amezungumzia kuhusu kile alichokiita , tukio baya, katika ushirikiano katika bara la Ulaya.

Sio wabunge wa bunge la Poland wala maafisa wawakilishi wa serikali walikuwa tayari kuzungumza na tume hiyo, amesema Coehlo.

Katika hali hii ningependa kueleza tofauti iliyopo ya ushirikiano nahisi kuwa kile tulichokiona hapa , ni kinyume kabisa na hali ya uwazi na ushirikiano tulioupata katika wiki tatu zilizopita tulipoitembelea Rumania na kile ambacho tumekumbana nacho wakati wa ziara yetu nchini Poland.

Hii ni muhimu, kwa sababu kama mjuavyo Poland na Romania , ni miongoni mwa nchi mbili za Ulaya ambazo zimetajwa kuwa zinadaiwa zilikuwa na vituo vya jela za siri.

Hapa kunajitokeza kama ilivyokuwa hapo kabla masuali mengi kwa Poland kutokana na mchezo huu. Baada ya uthibitisho wa mashahidi katika miaka iliyopita katika uwanja wa ndege uliofungwa wa Szymany, ndege kadha za binafsi za CIA zimekuwa zikitua. Kwa mfano ndege chapa Boeing 737 iliwahi mwezi Septemba 2003 kutoka katika mji mkuu wa Afghanistan Kabul kutua katika uwanja huo na baadaye kuendelea na safari kwenda Rabat nchini Morocco na hadi Guantanamo nchini Cuba. Ukweli huu huwezi kuutilia shaka ukiwa umetolewa na mkuu wa zamani wa usalama wa Poland Gromoslav Czempinski.

Kitu ambacho hakiko wazi ni kuwa ni jukumu gani inawezekana jeshi la Poland limechukua katika kazi hii ya msaada wa kijasusi katika uwanja huu wa ndege wa Szymany.

Wabunge wa umoja wa Ulaya wanadhani nyaraka kadha zimetoweka za orodha ya wasafiri wa ndege kutokana na ukimya wa maafisa wa nchi hiyo.

Kisiasa usanii huu hauisaidii hata kidogo nchi hiyo mwanachama wa umoja wa Ulaya, amesema mwenyekiti wa tume hiyo ya uchunguzi Coelho kuwa nafasi zote ziko wazi.

Kama itathibitika kuwa kulikuwa na utaratibu wa kuendea kinyume haki za binadamu katika nchi moja mwanachama wa umoja wa Ulaya , tutatumia kifungu cha saba cha mkataba. Lakini nataka kusema pia kuwa vikwazo ni suala la mwisho kabisa ambalo tunaweza kulizungumzia, baada ya kumaliza kazi yetu.

Inatarajiwa kuwa mwishoni mwa mwezi huu tume hiyo ya uchunguzi ya bunge la Ulaya itatoa rasmi ripoti yake ya mwisho.