1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Polisi wa Kenya wapambana na waandamanaji.

1 Aprili 2008
https://p.dw.com/p/DYqd

Nairobi.

Polisi wa Kenya wamefyatua mabomu ya kutoa machozi kwa karibu waandamanaji 100, ikiwa ni pamoja na mshindi wa tuzo ya amani ya Nobel waliokuwa wakiandamana mjini Nairobi kupinga pendekezo la ongezeko la idadi ya nafasi za baraza la mawaziri.

Wanasiasa ambao wamekubali kugawana madaraka ili kutuliza mzozo mkubwa wa uchaguzi wamependekeza kuongezwa kwa idadi ya nafasi za baraza la mawaziri ili kukidhi matakwa ya vyama.

Waandamanaji wamesema kuwa Kenya haiwezi kumudu gharama za wafanyakazi wa serikali wanaohitajika katika wizara hizo mpya, ambao wanalipwa karibu sawa na wafanyakazi wa Ulaya.