1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Polisi wavisaka vitongoji vya Paris

18 Februari 2008
https://p.dw.com/p/D9JE
Maafisa wa polisi zaidi ya 1,000 wameivamia miradi ya ujenzi wa makazi katika kitongoji cha mji mkuu Paris katika juhudi za kuwatafuta waandamanaji walioongoza machafuko ya mwaka jana. Watu takriban 25 wamekamatwa katika kitongoji cha Villiers le Bel kaskazini mwa Paris na wamepelekwa katika kituo cha polisi ili wahojiwe. Polisi wametawanywa katika vitongoji vingine vitatu wakati wa msako huo uliofanywa leo asubuhi. Maafisa wa polisi takriban 100 walijeruhiwa wakati wa machafuko ya mwezi Novemba mwaka jana yaliyozuka kufuatia vifo vya vijana wawili waliouwawa katika ajali iliyohusisha pikipiki na gari la polisi.