1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Pope awasili Mexico

24 Machi 2012

Kiongozi wa kanisa Katoliki duniani Pope Benedict ,16,amewasili nchini Mexico huku akilakiwa na mamia ya waumini waliojipanga kwa kiasi cha umbali wa kilometa 20 katika njia aliyopitia katika mji mkuu wa nchi hiyo.

https://p.dw.com/p/14Qwc
Pope Benedict XVI waves as he boards his plane to leave for his pastoral visit to Mexico and Cuba, at Fiumicino International Airport in Rome March 23, 2012. Pope Benedict begins his first visit to Mexico on Friday with the Roman Catholic faithful hoping he will deliver a strong message of peace to temper a brutal drugs war in the deeply religious country. REUTERS/Max Rossi (ITALY - Tags: RELIGION)
Kiongozi wa kanisa Katoliki duniani , Benedict XVI akiwasili MexicoPicha: Reuters

Waumini hao walikuwa wakiimba nyimbo za kumkaribishaPope Benedict huku wakisema, Benedict, kaka, sasa wewe ni Mmexico.

Wengi wanafikiri makaribisho hayo mazuri, yakisindikizwa na muziki wa asili, wa Mariachis , usingepaswa kumlaki kiongozi huyo wa kidini kwa kuwa unaonekana kuwa nje ya maadili ya kidini na wa kisomi tu. Lakini nchi hiyo yenye idadi kubwa ya waumuni wa kanisa Katoliki duniani, inayozungumza lugha ya Kihispoaniola, imemuonyesha papa Benedict mapenzi waliyonayo kwa mrithi wa kiti alichokalia pope John Paul wa 11, ambaye alionekana kuwa papa wa Mexico , wakati wa uhai wake baada ya kufanya ziara mara tano nchini humo.

Hii ni nchi yenye kujisikia fahari kwa ukarimu, na hakuna mtu ambaye anahisi kuwa mgeni katika nchi yenu, amesema papa wakati alipowasili huku akishangiliwa kwa nguvu.

Source News Feed: EMEA Picture Service, Germany Picture Service Pope Benedict (3rd L) is welcomed by Mexican President Felipe Calderon (2nd L) and his wife, after the Pontiff arrived at the Guanajuato International Airport at the start of his trip to Mexico March 23, 2012. Pope Benedict landed in Mexico on Friday promising to send out a strong message against drug cartels in a country convulsed by a surge in gang violence over the past five years. REUTERS/Tony Gentile (MEXICO - Tags: RELIGION) eingest. sc
Pope akisalimiana na waumini MexicoPicha: reuters

Nililifahamu hilo, na sasa naliona na nalihisi katika moyo wangu ameongeza pope Benedict.

Baada ya ndege yake kutua , mitaa ya Leon ambako pope atakaa , ilikuwa katika hali ya sherehe kubwa , ambapo majengo yote yaliripuka kwa kumwagiwa konfeti za rangi ya njano wakati akipita katika gari yake ambayo haiwezi kuathirika kwa bomu katika njia hiyo yenye urefu wa kilometa 32 kutoka uwanja wa ndege.

Amekuja kuwabadilisha Wamexicani wote, amesema Maria del Rosario Tamayo Villanueva, ambaye alitaka kumuona pope licha ya kuwa na ulemavu wa miguu yake yote tangu akiwa mtoto. Ilikuwa ni muhimu kuja kumuona. Ni zawadi kutoka kwa Mungu.

Pope Benedict (C) is welcomed by Mexican President Felipe Calderon (R) and his wife Margarita Zavala after the Pontiff arrived at the Guanajuato International Airport at the start of his trip to Mexico March 23, 2012. Pope Benedict landed in Mexico on Friday promising to send out a strong message against drug cartels in a country convulsed by a surge in gang violence over the past five years. REUTERS/Tony Gentile (MEXICO - Tags: RELIGION POLITICS) (eingest. SC)
Pope Benedict (katikati)akiwa na rais wa Mexico Felipe Calderon na mkewe Maria del Rosario TamayoPicha: Reuters

Hapo mapema katika safari yake ya saa 14 kutoka mjini Rome, Benedict amewataka Wamexicani kupambana na hali ya kuabudu fedha , hali ambayo inasababisha ghasia zinazohusishwa na madawa ya kulevywa na kuitaka Cuba, ambako anaelekea huko siku ya Jumatatu, kuachana na nadharia za Kimaxi, ambazo zimepitwa na wakati.

Amezungumzia hapo kabla upinzani wake dhidi ya biashara ya madawa ya kulevywa, nadharia za kimaxi pamoja na udikteta katika eneo la Latin America, ikiwa ni pamoja na katika ziara yake ya mwaka 2007 nchini Brazil, ikiwa ni ziara yake ya kwanza katika eneo hilo.

Siku ya Ijumaa rais wa Mexico Felipe Calderon na mkewe Margareta Zavala walimlaki Pope katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Guanajuto mjini Silao na kufuatana naye katika zulia jekundu huku kengele za kanisani zikilia.

Benedict aliteremka katika ngazi bila ya kutumia fimbo ambayo amekuwa akiitumia wakati alipoelekea katika ndege mjini Rome, ikiwa ni mara ya kwanza kutembea na fimbo hiyo hadharani.

Mwandishi : Sekione Kitojo / ape

Mhariri: Ndovie, Pendo Paul

Mhariri. Pendo Ndovie