1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Pope Benedict awataka viongozi kutatua mizozo.

26 Desemba 2007
https://p.dw.com/p/CgHz

Vatican.

Kiongozi wa kanisa Katoliki duniani Pope Benedict 16 ameadhimisha sikukuu ya Christmas kwa kutoa wito kwa viongozi wa kisiasa duniani kote kutafuta busara na nguvu za kumaliza mizozo katika maeneo kama Darfur, Iraq , Afghanistan na Congo. Benedict alisoma hotuba yake ya kila mwaka ya urbi et orbi kutoka katika baraza ya kanisa la St. Peters basilica mjini Vatican.

Kiongozi huyo wa kidini pia amelitaka kundi la watu waliohudhuria kumsikiliza kufurahia sherehe za kuzaliwa kwa Yesu, ambapo amesema anamatumaini , zitawaliwaza wale wote ambao wanaishi katika giza la umasikini, ukosefu wa sheria na vita.