1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

PORT HARCOURT:Uchaguzi wa magavana wakamilika

15 Aprili 2007
https://p.dw.com/p/CC9h

Raia wa Nigeria wamepiga kura hapo jana ili kuhakikisha kuwa demokrasia inadumishwa.Visa vya kuiba kura vilevile dosari nyingine zinaripotiwa kufanyika katika uchaguzi huo katika eneo la mafuta mengi la kusini.Yapata watu 17 wamepoteza maisha yao katika shughuli hiyo.Uchaguzi huo wa magavana unaazimia kutathmini uwezo wa tume ya uchaguzi huku wakijiandaa kwa uchaguzi wa Rais Aprili 21.Uchaguzi huo wa rais ni wa kwanza kufanyika kati ya wagombea wawili walio uongozini nchini humo.

Rais Olusegun Obasanjo alikubali kuwa ghasia zilitokea katika baadhi ya maeneo.