1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Putin: hatua ichukuliwe kashfa ya doping nchini Urusi

12 Novemba 2015

Rais wa Urusi Vladimir Putin amemuru uchunguzi ufanywe kuhusiana na madai kwamba wanariadha nchini humo walitumia dawa zilizipigwa marufuku michezoni

https://p.dw.com/p/1H4Qc
Russland Wladimir Putin in Sotschi
Picha: Reuters/A. Druzhinin

Putin ameyasema hayo ikiwa ni mara ya kwanza tangu tume huru ya Shirika la Kimataifa la Kukabiliana na Matumizi ya Dawa za Kusisimua Misuli - WADA kutoa ripoti yake iliyoonyesha kukithiri kwa matumizi ya dawa hizo nchini Urusi

Rais huyo wa Urusi ametaka kuwepo “ushirikiano” kati ya nchi yake na mashirika ya kupambana na matumizi ya dawa hizo zilizopigwa marufuku michezoni. “Kinyang'anyiro lazima kiwe wazi,” alisema Putin. “Shindano lolote la michezo linaweza tu kuvutia iwapo litakuwa wazi.” Amesema Putin.

Waziri wa michezo wa Urusi Vitaly Mutko awali alisema mfumo wa kukabiliana na dawa za kusisimua misuli Uingereza ni mbaya zaidi hata kushinda wa Urusi, madai ambayo yamekanushwa na Wizara ya michezo na utamaduni ya Uingereza

Putin amemtaka waziri wa michezo wa Urusi na wote wanaohusika kwa njia moja au nyingine na michezo kuangazia suala hili kikamilifu. Rais wa IAAF Sebastian Coe, ameliambia shirikisho la riadha la Urusi kujibu madai yote dhidi yake haraka iwezekanavyo

Mwandishi: Bruce Amani/AFP/Reuters
Mhariri: Mohammed Abdul-Rahman