1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Pyongyang.Korea ya Kaskazini yakubali kushiriki mazungumzo ya pande sita.

31 Oktoba 2006
https://p.dw.com/p/CCxK

Korea ya Kaskazini imeripotiwa kukubali kurejea katika mazungumzo yanayoshirikisha nchi sita kuhusiana na mpango wake wa kinyuklia.

Shirika la habari la Korea ya Kusini Yonhap limeripoti kuwa, makubaliano hayo yamefikiwa baada ya mkutano uliofanyika mjini Beijing kati ya maafisa wa Korea ya Kaskazini, China na Marekani.

Nalo shirika la habari la China Xinhua limearifu kwamba mazungumzo hayo yatafanyika siku za hivi karibuni, hata hivyo hakukuwa na taarifa zaidi juu ya mkutano huo.

Haya yamekuja wiki tatu tu baada ya Korea ya Kaskazini kujinasibu kuwa imefanikiwa katika jaribio lake la kinyuklia.

Korea ya Kaskazini ilijitowa katika mazungumzo ya pande sita mwaka mmoja uliopita, ikilalamika dhidi ya vikwazo vya kiuchumi ilivyowekewa na Marekani.