1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

QUITO: Waziri wa Ulinzi wa Ecuador afariki dunia kwenye ajali ya helikopta.

25 Januari 2007
https://p.dw.com/p/CCY7

Waziri wa kwanza wa ulinzi mwanamke wa Ecuador, Bibi Guadalupe Larriva, amefariki kwenye ajali ya helikopta siku tisa baada ya kuteuliwa kuwa waziri.

Maafisa wa kijeshi pamoja na serikali wamesema waziri huyo na binti yake walifariki jana baada ya helikopta mbili kogangana.

Ajali hiyo ilitokea karibu na kituo cha kijeshi kwenye pwani ya bahari ya Pasifik.

Bibi Guadalupe Larriva alikuwa mmojawapo wa mawiziri maarufu zaidi kwenye serikali ya Rais Rafael Correa.