1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Raia wa kigeni auwawa

2 Septemba 2007
https://p.dw.com/p/CBTT

LAGOS:

Raia wa kigeni amepigwa risasikatika mji wenye visima vya mafuta wa Port Hercourt,nchini Nigeria.Kisa hiki kinaonekana kama ni cha kulipiza kisasi-kwa muujibu vile polisi ilivyoarifu mjini Lagos.

„wauaji wameacha taarifa juu ya mwili wa mtu huyo wakidai walimpa dala 50.000 kuagiza magari kutoka Ulaya,lakini hakuwarejeshea fedha hizo wala kuwapatia motokaa hizo.“

Polisi iliarifu.

Maiti hiyo iligunduliwa nje ya nyumba ya raia huyo wa kigeni mjini Port Hercourt na ikidhihirisha ameuliwa jana usiku.