1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Rais Al-Bashir achochea vita ?

18 Novemba 2007
https://p.dw.com/p/CIlu

KHARTOUM:

Waasi wa zamani wa kusini mwa Sudan leo wamemtuhumu rais Al bashir wa Sudan „kutishia na kuitisha vita“ katika hotuba yake alioitoa kwa heshima ya wanamgambo-shirika na serikali yake wanaotuhumiwa viutendo kadhaa vya kikatili.

Pagan Amum, katibu mkuu wa SPLM, amesema amehuzunishwa na matamshi ya rais al-Bashir jana jumamosi.Katika hotuba yake kali ya TV, rais Al-Bashir alipandisha jazba ya kisiasa katika misukosuko mbali mbali inayoikabili Sudan na jirani zake pamoja na changamoto kati ya serikali yake ya Khartoum na chama cha ukombozi wa kusini mwa Sudan (SPLM).

Rais al Bashiri amewataka wanamgambo wa PDF kufungua kambi za m azowezi na kuwakusanya wapiganaji wa mujahedeen sio kwa azma ya vita bali kujiweka tayari kwa chochote kitakachotokea.Hakutoa maelezo zaidi juu ya madhumuni yake.