1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Rais Al-Bashir wa Syria aitisha tena upatanishi wa Uturuki .

24 Desemba 2009

Israel yataka mazungumzo yasio na mwisho ?

https://p.dw.com/p/LCqK
Recep Tayyip Erdogan-waziri mkuu wa Uturuki azuru Syria.Picha: AP

Rais Bashar al-Assad wa Syria, ameituhumu Israel jana kuwa, inakwamisha mazungumzo ya amani na akapendekeza kuanzishwa upya juhudi za Uturuki za kupatanisha kati ya Syria na Israel.

Waziri-mkuu wa Uturuki, Tayyip Erdogan, anaezuru Uturuki ,amesifu usuhuba unaoimarika kati ya nchi yake na Syria.Hii inatokea wakati mahusiano kati ya Israel na Uturuki , yamechafuka tangu vita vya mwaka jana vya Gaza baina ya Israel na Hamas.

"Israel ndio chanzo kikuu cha kukwama kwa amani .Waisraeli wanataka mazungumzo ambayo yanakiuka kanuni za kimsingi.Hivyo ni kusema wanachotaka ni mazungumzo yasio na mwisho wake."-alisema Rais Bashar al-Assad katika mkutano na waandishi habari pamoja na mgeni wake waziri mkuu Tayyip Erdogan wa uturuki anaetembelea Syria.

Rais Assad akaongeza kusema kuwa, upatanishi wa Uturuki mwaka jana, ulikuwa wa dhati,usio na maonevu na kulingana na ukweli wa hali ya mambo." Akaongeza, "Tunahitaji sasa zaidi kuliko wakati wowote ule upatanishi huo."

Usuhuba mwema uliokuwapo baina ya Israel na Uturuki,umeharibika tangu pale serikali ya Uturuki ya chama cha kiislamu kuikosoa mno Israel kwa hujuma zake kali katika mwambao wa Gaza mwaka uliopita.Ghadhabu zilizozuka juu ya hujuma hizo za Israel zikagubika wingu lake juu ya mazungumzo baina ya Israel na Syria yalio simamiwa na Uturuki.

Waziri mkuu wa Uturiki kwa upande wake amepongeza mno mafungamano yanayozidi kati ya nchi yake na jirani yake Syria na akasema huo ni mfano wa kuigiwa na nchi nyengine za kiarabu.

"Tunapita kipindi cha kihistoria.Tutaziondoa pingamizi zote ziliopo njiani na kuunda pamoja na Syria, msingi wa kupigiwa mfano wa ushirikiano utakaweza kufuatwa na nchi nyengine."-alisema Erdogan.

Waziri mkuu wa uturuki alisema kwamba hivi sasa nchi yake inafanya juhudi za kupanua uhusiano na nchi nyengine za kiarabu pamoja nazo Iraq,Jordan na Lebanon.

Erdogan, anatumai biashara ya pande mbili kati ya Syria na Uturuki,itaongezeka kutoka kima cha sasa cha dala bilioni 2 kwa mwaka na kupanda hadi dala bilioni 5 mnamo miaka 3 hadi 4 ijayo.Usuhuba kati ya Syria na Uturuki, ulichafuliwa siku za nyuma na tuhuma za Uturuki, kuwa Syria, ikiwaunga mkono waasi wa chama cha wakurdi cha "Kurdistan Workers' Party" pamoja na mvutano juu ya chemchem za maji za mto Euphrates na madai ya zamani ya eneo la Hatay ambalo dola la kikoloni Ufaransa,liliipa Uturuki, hapo1938.

Mwandishi: Ramadhan Ali /AFPE

Uhariri: Yusuf Saumu