1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Rais Ali Abdullah Saleh wa Yemen atibiwa Saudi Arabia

5 Juni 2011

Hali nchini Yemen inaripotiwa kuwa shwari baada ya Rais Ali Abdullah Saleh kuwasili Saudi Arabia ili kupata matibabu.

https://p.dw.com/p/11UY4
Ramani ya YemenPicha: DW

Taarifa hizo zimethibitishwa na maafisa wa serikali ya Yemen na Saudi Arabia ambao hawakutaka kufahamika. Duru zinaeleza kuwa baadhi ya maafisa wengine wa ngazi za juu wa serikali ya Yemen nao pia wameeleka Saudi Arabia kutibiwa baada ya  eneo  la  kasri ya Rais Saleh kushambuliwa kwa roketi iliyofyatuliwa na waasi Ijumaa iliyopita wakati wa usiku. 

Jemen Präsident Ali Abdullah Saleh NO FLASH
Rais Ali Abdullah Saleh: Taarifa zaeleza kuwa ameteketea na ana majeraha karibu na moyoPicha: AP

Wahudumu wa usalama wanaripotiwa kuwa waliuawa katika shambulio hilo. Kwa upande mwengine, taarifa za shirika la utangazaji la BBC zinaeleza kuwa Rais Ali Saleh huenda ameteketea vibaya na kupata majeraha karibu na moyo, baada ya shambulio hilo. Katika hotuba yake ya Ijumaa jioni iliyotangazwa na kituo cha redio ya taifa, Rais Saleh alisema hana neno.

Flash-Galerie Continuous anti-government protests in Yemen
Wapinzani wa Rais Saleh wakisherehekea baada ya kiongozi huyo kuelekea Saudi ArabiaPicha: picture alliance / dpa

 Itakumbukwa kuwa wapinzani wa kiongozi huyo wa Yemen, wamekuwa wakiandamana kwa muda mrefu ili kumshinikiza aondoke madarakani hasa baada ya Rais Saleh kukataa katakata kulitia saini pendekezo lililotolewa na Baraza la Mataifa ya Ghuba, GCC. Kulingana na pendekezo hilo, Rais Saleh anapaswa kuachia ngazi pasina adhabu ya mahakama. 

Mwandishi: Mwadzaya, Thelma-ZPR

Mhariri: Kitojo, Sekione

Ruka sehemu inayofuata Gundua zaidi