1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Rais Bush akamilisha ziara yake barani Afrika

22 Februari 2008
https://p.dw.com/p/DBS5

MONROVIA:

Rais wa Marekani George W.Bush ameondoka Liberia,akikamilisha ziara yake ya siku sita iliyompeleka katika nchi tano barani Afrika.Hapo awali alikuwa na mazungumzo pamoja na Rais wa Liberia Bibi Ellen Johnson Sirleaf.Bush hakuthibitisha ripoti zilizosema,Liberia huenda ikaruhusu kikosi maalum cha Marekani kwa bara Afrika-AFRICOM kuwa na makao yake makuu nchini humo.Vile vile alipuza hofu za kuwepo ushindani kati ya China na Marekani kuhusu raslimali za bara Afrika kama vile mafuta na madini.

Wakati wa ziara hii iliyompeleka pia nchini Benin,Tanzania,Ghana na Rwanda,Rais Bush ameahidi msaada wa zaidi ya Dola bilioni moja kupiga vita umasikini,malaria na UKIMWI.