1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Trump na Putin kukutana hivi karibuni mjini Paris

Amina Mjahid
24 Oktoba 2018

Rais wa Urusi Vladimir Putin anatarajiwa kukutana na rais wa Marekani Donald Trump baada ya Trump kutishia kuwa Marekani itajiondoa katika mkataba wa kudhibiti silaha za nyuklia kati ya Urusi na Marekani, INF.

https://p.dw.com/p/375jQ
Helsinki Trump-Putin Gipfel
Picha: Reuters/K. Lamarque

Kufuatia kitisho hicho cha Marekiani kujiondoa katika mkataba wa kudhibiti silaha za nyuklia kati ya Urusi na Marekani INF, Rais Putin amesema anataka kukutana na rais wa Marekani Donald Trump kwa mazungumzo mjini Paris.

Tangazo la kushtukiza la Trump kujiondoa katika mkataba huo limesababisha hisia mbali mbali kutoka kwa viongozi wa mataifa ya Ulaya.

John Bolton
Picha: Getty Images/M. Ngan

Katika mkutano na  mshauri wa masuala ya usalama wa taifa wa Marekani John Bolton, mjini Moscow Putin alisema yuko tayari kukutana na Trump hivi Karibuni. Wawili hao wanatarajiwa kuonana tarehe 11 Novemba pembezoni mwa sherehe za kuadhimisha miaka 100 ya kumalizika kwa vita vya kwanza vya dunia.

Bolton aliekuwa ziarani nchini Urusi amezungumzia mustakabali wa mkataba huo na waziri wa mambo ya kigeni wa Urusi Sergey Lavrov pamoja na mkuu wa baraza la usalama la Urusi Nikolai Patrushev.

Baada ya kukutana na Bolton, Patrushev alisema Urusi iko tayari kufanya kazi na Marekiani ili kuuokoa mkataba huo.

Katibu Mkuu wa NATO Jens Stoltenberg asema washirika wote wa Ulaya wanakubali kuwa mkataba huo ni muhimu.

"Washirika wote wanakubali kuwa mkataba huu ni muhimu ndio maana tuna wasiwasi juu ya tabia ya Uru

Kwa upande wake Katibu Mkuu wa NATO Jens Stoltenberg amesisitiza uwepo wa mkataba  huo wa nyuklia kati ya Urisi na Marekani ambapo Marekani imesema mkataba huo umekiukwa na Urusi. Mkataba huo uliotiwa saini mwaka 1987 unapiga marufuku makombora ya nyuklia kurushwa kwa zaidi ya umbali wa kilomita 5,500.

Lakini Marekani inadai Urusi imekiuka hilo kwa kombora lililorushwa mapema mwaka huu. Stoltenberg  anasema washirika wote wa Ulaya wanakubali kuwa mkataba huo ni muhimu .

Belgien Nato-Verteidigungsministertreffen in Brüssel
Picha: Reuters/F. Lenoir

"Washirika wote wanakubali kuwa mkataba huu ni muhimu ndio maana tuna wasiwasi juu ya tabia ya Urusi kwahiyo tatizo ni tabia ya Urusi ambayo tumeiona kwa miaka mingi hii haiwezi kuendelea hatuwezi kuwa na mkataba kati ya pande mbili na inaheshimiwa tu na pande moja,” alisema Stoltenberg.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Ujerumani, Heiko Maas amesema mkataba huo ni nguzo muhimu kwa usalama wa Ulaya, lakini waziri wa Ulinzi wa Uingereza, Gavin Williamson amesema taifa hilo lipo pamoja na Marekani kutokana na Urusi kuyadhihaki makubaliano hayo.

Rais wa Poland Andrzej Duda amesema tangazo la Trump la kujiondoa katika mkataba huo linaeleweka kufuatia shughuli zinazofanywa na Urusi.

Mwandishi: Amina Abubakar/AP/dpa

Mhariri: Iddi Ssessanga