1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Rais Gbagbo aapishwa

Kabogo Grace Patricia4 Desemba 2010

Rais huyo ameapishwa rasmi kuiongoza Ivory Coast, licha ya jumuiya ya kimataifa kukataa kutambua ushindi wake.

https://p.dw.com/p/QPmh
Rais wa Ivory Coast, Laurent Gbagbo.Picha: Picture-Alliance/dpa

Rais aliyeko madarakani nchini Ivory Coast, Laurent Gbagbo ameapishwa rasmi kuiongoza nchi hiyo, licha ya ushindi wake kukataliwa na viongozi wa dunia. Hata hivyo, ushindi huo unakubalika na jeshi, hivyo kuzusha hofu kuhusu mapambano ya madaraka.

Tume ya Uchaguzi ya Ivory Coast ilimtangaza mpinzani wa Gbagbo, Alassane Ouattara kama mshindi wa uchaguzi wa rais wa Novemba 28 kwa kupata asilimia 54.1, lakini Baraza la Katiba lilimtangaza Gbagbo kuwa mshindi.

Wakati huo huo, Waziri Mkuu wa Ivory Coast, Guillaume Soro leo amesema anaamini kuwa Ouattara alishinda katika uchaguzi huo na sio Gbagbo, hivyo atajiuzulu wadhifa huo baada ya Gbagbo kuapishwa.

Aidha, katika hatua nyingine watu wawili wameuawa katika mapigano makali baada ya vikosi vya usalama kufyatua risasi katika mji wa Abidjan. Mauaji hayo yametokea katika wilaya ya Port-Bouet kusini mwa Abidjan wakati vikosi vya usalama vilipofyatua risasi wakati wa mapigano baina ya wafuasi wa Gbagbo na Ouattara.

Mwandishi: Grace Patricia Kabogo (RTRE,AFPE)

Mhariri: Mohamed Dahman