1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Rais Hamid Karzai aongoza kwa mara ya pili

Thelma Mwadzaya17 Septemba 2009

Ujerumani imesisitiza kuwa matokeo ya uchaguzi wa rais ya Afghanistan ni ya muda mpaka pale madai ya hila na udanganyifu yatakapochunguzwa kikamilifu.

https://p.dw.com/p/JiWA
Waangalizi wa Uchaguzi wa EU,AfghanistanPicha: DW

Kulingana na waangalizi wa uchaguzi wa Umoja wa Ulaya walioko nchini Afghanistan kiasi cha kura milioni 1.5 huenda zilikuwa na hila.

Kulingana na matokeo ya muda yaliyotangazwa na Tume ya Uchaguzi ya Afghanistan baada ya kuzihesabu upya baadhi ya kura zilizopigwa Rais Hamid Karzai amepata takriban asilimia 55 ya kura zote.Mpinzani wake mkuu Abdullah Abdullah anaripotiwa kuwa amepata kiasi cha asilimia 28 ya kura zote.Hali hiyo imeifanya Tume ya Uchaguzi inayohusika na matatizo ya uchaguzi imeamrisha kiasi cha asilimia 10 ya kura zote kuhesabiwa upya.

Thelma Mwadzaya/ AFPE,DPAE