1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Rais Kabila ziarani Ubeligiji

23 Septemba 2007
https://p.dw.com/p/CBNG

Brussels:

Rais Joseph Kabila wa jamhuri ya kidemokrasi ya Kongo amewasili Brussels hii leo kwa ziara ya siku mbili nchini Ubeligiji.Rais Kabila amepangiwa kuzungumza jioni hii na viongozi wa serikali ya jimbo la Wallonie pamoja pia na waziri mkuu wa jumuia ya wenye kuzungumza kifaransa nchini Ubeligiji bibi Marie Anne.Mahala mazungumzo hayo yatakakofanyika ni siri kwasababu ya hofu ya kuzuka maandamano ya wapinzani wa rais Kabila.Kesho kiongozi huyo wa jamhuri ya kidemokrasi ya Kongo atakutana na viongozi wa serikali inayomaliza wadhifa wake ,ikiwa ni pamoja na waziri mkuu Guy Verhofstadt na waziri wa mambo ya nchi za nje Karel De Gucht.Rais Joseph Kabila,anaeitemebela Ubeligiji kwa mara ya kwanza tangu mwaka 2004,yuko njiani kuelekea New-York ambako atahudhuria mkutano wa baraza kuu la Umoja wa mataifa.