1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Rais Kagame asifu opereshini za pamoja

Oumilkher Hamidou24 Januari 2009

Kinshasa yataka Laurent Nkunda arejeshwe

https://p.dw.com/p/GfVt

Kinshasa/Kigali:

Rais Paul Kagame wa Rwanda amesifu "matokeo mema" ya opereshini inayoendeshwa na wanajeshi wa jamhuri ya kidemokrasi ya Kongo na Rwanda dhidi ya waasi wa Rwanda katika eneo la mashariki la jamhuri ya kidemokrasi ya Kongo.Akihutubia kupitia Radio Rwanda rais Kagame amesema "hajawahi kuwa na matumaini mema kama sasa."Hii ni mara ya kwanza kwa rais Kagame kuzungumzia hadharani opereshini  hiyo ya pamoja iliyoanzishwa january 20 dhidi ya waasi wa kihutu wa FDLR,pamoja pia na kukamatwa  mkuu wa waasi wa kitutsi Laurent Nkunda,alkhamisi iliyopita nchini Rwanda."Tunaendesha opereshini za pamoja ili kuvunja nguvu vyenzo vya mtafaruku,ugonvi na maafa katika eneo letu" amesema rais Kagabe kupitia Raio ya serikali ya Rwanda,alipokua akiwabushuria kheri ya mwaka mpya mabalozi wa nchi za nje.Wakati huo huo vyombo vya habari katika jamhuri ya kidemokrasi ya Kongo vinasifu opereshini hiyo iliyopelekea kukamatwa mkuu wa waasi wa kitutsi Laurent Nkunda.Mashirika yasiyo milikiwa na serikali yanamlaumu Nkunda kwa kuwabebesha silaha watoto wadogo.Serikali ya mjini Kinshasa inapigania Laurent Nkunda arejeshwe Kinshasa kujibu mashtaka ya uhalofu dhidi yake.Wanajeshi wa Rwanda na wale wa jamhuri ya kidemokrasi ya Kongo wanaendelea na opereshini yao mashariki mwa Kongo Kinshasa.