1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Rais Karume ateua wawakilishi wawili toka chama cha CUF

Kabogo Grace Patricia15 Desemba 2009

Hatimaye Rais Aman Abeid Karume wa Zanzibar amewateua wajumbe wawili wa chama cha upinzani CUF kujiunga na Baraza la wawakilishi.

https://p.dw.com/p/L33T
Rais Aman Abeid Karume wa Zanzibar.Picha: AP Photo

Kuteuliwa kwa Juma Duni na Nassoro Mazrui kunafuatia mazungumzo ya mara mbili kati ya Rais Karume na Katibu Mkuu wa CUF Seif Shariff Hamad na uamuzi wa chama hicho kumtambua rais huyo wa Zanzibar.

Grace Kabogo alizungumza na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Zanzibar inayoshughulika na utafiti na sera za kijamii, Mohammed Yusuf, na kwanza alimuuliza maoni yake juu ya hatua hiyo ya Rais Karume

Mahojiano: Grace Patricia Kabogo/Mohammed Yusuf

Mhariri:M.Abdul-Rahman