1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Rais Mugabe akiri kuwepo njaa nchini Zimbabwe

10 Machi 2008

Rais Robert Mugabe wa Zimbabwe amekiri kwa mara ya kwanza kwamba kuna njaa nchini mwake.

https://p.dw.com/p/DLXj

HARARE

Amekaririwa na gazeti linalodhibitiwa na serikali la Sundaya Mail akisema kwamba kuna njaa nchini humo na uhaba wa chakula.

Mugabe alikuwa akizungumza kwenye mkutano wa hadhara mwishoni mwa juma katika wilaya kame ya Plumtree magharibi mwa Zimbabwe kufuatia ombi kutoka kwa gavana wa jimbo Angelina Masuku na maafisa wa chama wa serikali ya mtaa ambao kwa mujibu wa gazeti hilo walimsihi Mugabe kuhakikisha usambaji chakula wa haraka katika jimbo hilo kwa vile wananchi wake wanaishiwa na chakula.

Wachunguzi wa mambo wamesema kukiri huko kwake hakukuwahi kufanya kabla kwa vile Mugabe huko nyuma amekuwa akizitupilia mbali repoti za kuwepo kwa njaa kuwa ni propanganda za mataifa ya magharibi.

Hapo mwaka 2006 wakati alipoulizwa kwenye mahojiano juu ya uhaba mkubwa sana wa mahindi chakula kikuu cha taifa alisema wana viazi chungu nzima.

Hapo jana Mugabe amekri kwamba kuna uhaba wa chakula sio tu kwenye majimbo ya magharibi yalio kama kwa muda mrefu ya Matebleland bali pia kwenye maeneo ya mashariki mwa Zimbabwe.