1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Rais Mugabe ashikilia atatangaza baraza bila upinzani

Ponda, Eric Kalume28 Agosti 2008

Nchini Zimbabwe, Rais Rais Robert Mugabe anatarajiwa kulitangaza Baraza lake la mawaziri hii leo. Hatua hii, hata hivyo, inapingwa vikali na upinzani wanaodai kuwa itakwamisha kabisa mashauri yanayokusudiwa kuundwa

https://p.dw.com/p/F6dp
Rais Robert Mugabe wa ZimbabwePicha: picture-alliance/ dpa


Tangazo la waziri mdogo wa habari nchini humo, Bright Matonga, kwamba Rais Mugabe anatarajiwa kulitangaza baraza lake la mawizi hii leo, limetonesha donda la kisiasa nchini humo, huku wafuasi wa chama Cha Movement for Democratic Change MDC wakimuonya vikali rais huyo dhidi ya kile wanachokitaja kuwa maamuzi ya Kibabe.



Katibu mkuu wa chama cha MDC, Tendai Biti, alisema hatua ya Rais Mugabe inakwenda kinyume kabisa na makubaliano ya hivi majuzi yaliyoafikiwa kati ya chama cha ZANU-PF na upinzani kuhusu kugawana mamlaka.


Licha ya onyo hilo kutoka kwa upinzani, Waziri Matonga alisema Serikali ya Mugabe ilipewa mamlaka na muungano wa mataifa ya Kusini mwa Africa, SADC, na kwamba hakuna kinachoweza kumuzuia Mugabe aunde baraza jipya la mawaziri.


Kwa Upande wake, katibu mkuu wa MDC, Tendai Biti, anasema iwapo Rais Mugabe ataendelea na hatua hiyo, basi asahau mashauri ya kuuundwa serikali ya Umoja wa Taifa nchini humo.

Tangazo hilo limetokea siku tatu tu baada ya kuapishwa bunge la nchini hiyo siku ya Jumatatu ambapo Rais Mugabe alizomewa bungeni. Mashauri ya kutafuta kuundwa serikali ya mseto nchini Zimbabwe, chini ya upatanishi wa Rais Thabo Mbeki wa Africa Kusini, yaliahirishwa wiki mbili zilizopita.


Bunge la Zimbabwe lilifunguliwa mapema wiki hii, miezi mitano baada ya uchaguzi uliokumbwa na dosari na ambao Rais Mugabe kwa mara ya kwanza tangu nchini hiyo ijipatie uhuru kwake mwaka 1980 kutoka kwa Uingereza, alishindwa vibaya na mpinzani wake, MorganTvsangirai. Hata hivyo, Rais Mugabe alishinda kiti hicho wakati wa duru ya pili ya uchaguzi uliosusiwa na mpizani wake, Morgan Tsvangira.


Mugabe amekuwa akiulaumu upinzani kama kibaraka na huenda hatua hii inalenga kuutenga upinzani katika kugfanya maamuzi muhimu serikali. Rais Mugabe mwenye Umri wa miakam 84 amesthumiwa vikali na hasa mataifa ya magharibi kwa sera zake sizisofungamana na mfumo wa kidemokrasia, huku akikabiliwa na tisho la kuwekewa vikwazo.


Mashauri hayo yalikwama baada ya kiongozi huyo wa MDC Morgan Tsvangirai kukutaa mpango wa kugawana mamlaka unaompa Rais Mugabe mamlaka zaidi ya kuwateua na kuwaafuta kazi mawaziri, na pia kuhusu suala tete la ni muda gani serikali hiyo itasalia mamlakani. Wadadisi wa masuala ya kisiasa wanasema kuwa huenda hii ni ishara kamili ya kukwama kwa mashauri hayo.


Msemaji wa Rais Thabo Mbeki ambaye ni mpatanishi mkuu kwenye mashauri hayo Mukoni Rat shitanga amesisitiza kwamba bado mashauri hayo yanaendelea ingawa hakutaja tarehe kamili ya kurejelewa kwa mashauri hayo.