1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Rais Musharraf ajiuzulu wadhifa wa mkuu wa jeshi la Pakistan

28 Novemba 2007
https://p.dw.com/p/CTz6

Rais Pervez Musharraf wa Pakistan anajiuzulu wadhifa wake kama kiongozi wa jeshi hii leo.

Hatua hiyo ni ishara kwamba rais Musharraf hatimaye amekubali miito ya jumuiya ya kimatiafa iliyomtaka amalize miaka minane ya utawala wa kijeshi uliokabiliwa na migawanyiko.

Katika juhudi ya kuondoa wasiwasi unaozidi kufuatia kutangaza hali ya hatari, rais Musharraf atakabidhi madaraka kwa naibu wake, jenerali Ashfaq Kiyani.

Pervez Musharraf ataapishwa kesho kuwa rais wa kiraia wa Pakistan.