1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Rais Obama ziarani nchini Uturuki

Nyajundi, Jason/ RTRE6 Aprili 2009

Anatarajiwa kuitaka Uturuki isaidie kuleta uthabiti Mashariki ya Kati

https://p.dw.com/p/HRBx
Rais Barack Obama alipokuwa akizungumza mjini Prague Jumapili Aprili 5Picha: AP

Rais wa marekani Barack Obama yuko nchi uturuki kuboresha zaidi uhusiano kati ya taifa hilo la kiislamu pamoja na Marekani, uhusiano ambao utairuhusu marekani kukabilaina na mizozo iliyopo Iraq na Afghanistan pamoja na uhusiano wake na Iran.

Mapema leo Jumatatu rais Obama alianza ziara yake kwa kulitembelea eneo la makumbusho na kuweka shahada la maua katika kaburi la mwanzilishi wa taifa la uturuki Mustafa Kemal Ataturk katika mji wa Ankara.

Ziara hii ya siku mbili nchini uturuki itakuwa ndiyo ya mwisho kwa rais Obama barani ulaya na kwanza katika taifa la kiislamu tangu aingie madarakani mwezi Januari mwaka huu.

Akiwa nchini Uturuki rais Obama pia atafanya mashauriano na rais wa uturuki Abdullah Gul pamoja na waziri mkuu Recep Tayyip Erdogan, ambapo pia atalihutubia bunge la uturuki, kwenye hotuba ambayo itachangia kutoa hakikisho kuwa Uturuki ni mshirika mkubwa wa marekani na taifa linalotambulika kuwa lenye umuhimu barani ulaya.

Uturuki, taifa pekee la kiislamu mwanachama wa jumuiya ya kujihami ya NATO, amekuwa mshirika wa karibu wa marekani likiwa ni taifa linalotenganisha ulaya pamoja na mashariki ya kati pamoja na nchi zinazokabiliwa na mzozo, zikiwemo Georgia , Iraq , Iran na Syria.

Uhusiano kati ya uturuki na marekani uliharibika wakati wa kipindi cha utawala wa ais George Bush, baada ya uturuki kukataa kuruhusu vikosi vya marekani kutumia ardhi yake, wakati marekani ilipoongoza uvamizi nchini Iraq mwaka 2003.

Huku Uturuki ikiwa jiran wa Iraq, rais Obama atahitaji pia kufanya mashauri ya kuiomba uturuki kuruhusu vituo vyake vya kijeshi kutumika kwenye mpangp wa marekqani wa kuondoa vikosi vyake kutoka Iraq.

Hata hivyo Uturuki huenda pia ikawa na umuhimu mkubwa kwa marekani wakati inahitajika kuwa kiungo muhimu kuyashawishi mataifa mengine kuruhusu vituo vyao kutumiwa na marekani, wakati inapojiandaa kupeleka vikosi zaidi nchini Afghanistan.

Katika miaka ya hivi karibuni ilionekana kuwa uturuki ilikuwa ikijitenga na sera za marekani katika masula kadha yakiwemo mipango ya nyuklia ya Iran , suala la kundi la Hamas katika katika mashariki ya kati pamoja na mzozo nchini Sudan, hali ambayo ilizua hofu kuwa huenda uturuki ilikuwa ikijitenga zaidi kutoka kwenye nchi za magharibi.

Hata hivyo matamshi ya ruis Obama kwenye mkutano wa jumuiya ya nchi za ulaya mjini Prague, ambapo aliunga mkono kujiunga kwa uturuki katika jumuiya yalipüingwa na rais wa ufaransa Nicholas Sarkozy.

Kwenye mzozo katika mashariki ya kati, uturuki itakuwa yenye umuhimu ikizingatiwa kuwa ina uhusinno mzuri na kundi la Hamas na huenda ikawa na imchango mkubwa wakati Marekani inapofanya juhudi za kutafuta amani kati Israel na palestina.

Mwandishi JASON NYAKUNDI/RTR

Mhariri MOHAMMED ABDULRAHMAN