1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Rais Perves Musharraf kuiondoa hali ya hatari

Siraj Kalyango30 Novemba 2007

Wapinzani wake sasa wamechangayikiwa hajui la kufanya

https://p.dw.com/p/CV4M
Rais Perves Musharraf asema amri ya hali ya hatari kuondolewa 16 Disemba 2007Picha: AP

Rais Perves Musharraf wa Pakistan inasemekana anapanga kuiondoa hali ya hatari nchini mwake Disemba 16 . Na hatua hiyo imewafurahisha marafiki zake wa nchi za magharibi.

Marekani, mshirikka mkuu wa rais Musharraf,imeulezea mpango wa kiongozi wa sasa Pakistan wa kuondoa amri ya hali ya hatari alioitangaza wiki kadhaa zilizopita,kama hatua moja muhimu.Hata hivyo imeongeza kuwa baado kuna hatua fulani zilizosalia, ili kuifanya Pakistan kurejea katika njia ilioiita,utawala wa demokrasia ya kikatiba.

Aidha imemuomba kuwakubalia wanaomkosoa kutoa maoni yao na kuhakikisha uhuru wa vyombo vya habari,kama ulivyokuwa kabla ya kuitangaza hali ya hatari.

Akikaribisha tangazo la Bwana Musharraf alilofanya jana kupitia televisheni, msemaji wa Ikulu ya White House, Dana Perino amebaini kuwa rais Bush, ameitaja hatua ya sasa ya Bwana Musharaf kama hatua muhimu ya kuirejesha Pakistani katika njia ya demokrasia.

'...nafikiri ntampongeza rais Musharrfa hapa kwani alipochukua uamuzi wa kutangaza hali ya hatari,ambayo luliamini kuwa ilikuwa kosa, alichukua hatua ya kuwa siliana na kuwasiliana nae na nafikri alichukua uamuzi yeye mwenyewe'. amesema Perino.

Aidha msemaji wa Ikulu ya Marekani amemhimiza Musharraf kuhakikisha kuwa wanaomkosoa wanakubaliwa kufanya mikutano ili kutoa maoni yao.

Rais George W. Bush ambae ni rafiki mkubwa wa Musharraf anasema kuwa amemsisitizia mwenzake kuwa wao wanataka demokrasia kamili.

...'nilizungumza na rais Musharraf na ujumbe wangu kwake ulikuwa,sisi tunaamini uchaguzi mkuu na kuwa utafanyika hivi karibuni na kuwa ni lazima uvue sare za kijeshi,'asema Bush.

Miongoni mwa yale Musharraf aliosema katika hotuba yake ni kuwa ataondoa hali ya hatari Disemba 16 , nakuongeza kuwa uchaguzi mkuu utafanyika kwa mujibu wa katiba ya nchi na utakuwa wa huru na wa haki.Pia amewataja wapinzani wake wakuu wa kisiasa kama vile Bi Benazir Bhutto pamoja na Nawaz Sharrif waliokuwa uhamishoni sasa kuwa wamerejea nyimbani. Amewahimiza kushiriki katika uchaguzi kikamilifu na kwa kufuata kanuni zitakazowekwa na tume kuu ya uchaguzi.