1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Jumuiya ya Kimataifa lilipinga kunyakuliwa kwa Golan.

Faiz Musa 22 Machi 2019

Rais wa Marekani Donald Trump ameahidi kuitambua milima ya Golan kama eneo lililo chini ya miliki ya taifa la Israel, Milima hiyo ilichukuliwa na Israel kutoka Syria mnamo vita vya Mashariki ya Kati vya mwaka 1967.

https://p.dw.com/p/3FWNf
Israel Syrien Golanhöhen
Picha: Imago/Xinhua

Israel iliikamata milima hiyo ya Golan katika vita vya siku sita mwaka 1967 na mwaka 1981 ikaitangaza kuwa eneo lake, hatua ambayo haikutambuliwa na jumuiya ya kimataifa. Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa lilipitisha azimio la kupinga kunyakuliwa kwa milima ya Golan, na  badala yake kupendekeza mazungumzo baina ya Syria na Israel.

Mwaka 1973 Syria ilishindwa kupata udhibiti wa eneo hilo la Golan katika vita vingine kati ya nchi za Kiarabu na Israel, vita hivyo vilisimamishwa kwa muda na kisha waangalizi wa umoja wa mataifa kulazimisha kusitishwa kikamilifu.

Mara kadhaa mazungumzo ya amani baina ya Israel na Syria yamegonga mwamba huku Syria ikitaka kurudishwa kwa eneo lote lililochukuliwa na Israel ndio waweze kuingia katika makubaliano ya baadaye ya amani.

Syrien Golanhöhen Versammlung der Religionsgemeinschaft der Drusen
Watu wa jamii ya Druze wakiwa Majdal Shams eneo la GolanPicha: Reuters/A. Awad

Sehemu ya Milima ya Golan kunaishi kiasi cha watu elfu arobaini kiasi cha nusu yao ni Wayahudi na wengine ni jamii ya Druze na jamii ndogo ya Alawi.

Druze ni waarabu waisilamu wanaojitambua kama Wasyria na Waalawi ni wa madhehebu ya Shia. Rais wa Syria Bashar Assad na viongozi wengi wakuu wa serikali yake wanatoka katika jamii hiyo.

Eneo la Golan ni mlima ulio na ukubwa wa kilomita 1,200 za mraba unaonekana hadi Lebanon, Syria na katika bonde la nchi ya Jordan.

Israel - Syrien Golan-Höhen
Kambi ndogo ya jeshi la Israel ikionekana juu ya milima ya GolanPicha: Getty Images/AFP/J. Eid

Sehemu ulipo ni kilimota 60 kutoka mji mkuu wa Syria, Damascus na unaipa Israel sehemu muhimu ya kujilinda na vile vile kuona vikosi vya majeshi vinavyopita maeneo hayo, hili linamaanisha lau Syria itathibiti eneo hili basi nayo itakuwa na nafasi nzuri ya kiusalama dhidi ya Israel kwa kuweza kuona kwa juu yanayoendelea Israel.

Katika eneo hilo la Golan kunapatika chanzo kikubwa cha maji kwa mto Jordan na bahari ya Galilea ambayo ni chanzo kikuu cha maji kwa taifa la Israel. Zaidi ardhi yake ina rutuba na inatumika kwa kilimo, kunapatikana mizabibu na bustani.

Kitendo cha rais Trump kusema Marekani inafaa kulitambua eneo la Golani kuwa sehemu ya Syria kinaweza kuweka mfano mbaya wa kwamba mataifa yanaweza kunyakua sehemu za mataifa mengine katika vita kinyume cha sheria za kimataifa.

Golanhöhen Schnee am Mount Hermon
Sehemu ya kufanya michezo ya kuteleza kwenye barafu GolanPicha: Benjamin Hammer

Azimio la Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa lililoungwa mkono na hata Marekani liliweka msingi wa kisheria unaosema Israel kuchukua eneo la Syria ni kukiuka sheria za kimataifa.

Vita vya wenyewe kwa wenyewe nchini Syria vimeidhoofisha nchi hiyo jambo linaloipa Israel nafasi nzuri ya kuzidi kudai eneo hilo.

Mada ya Golani ni hoja kuu sasa kutokana na kwamba serikali ya mrengo wa kulia ya Israel ina urafiki na utawala wa Trump ambao tayari mwaka 2017 uliutambua mji wa Jerusalem kama mji mkuu wa Israel na vile vile kuhamishia huko ubalozi wa Marekani.

Kauli ya Trump ya kuhusu milima ya Golan imetafsiriwa kuwa yenye nia ya kumsaidia zaidi waziri mkuu Benjamin Netanyau katika kinyang'anyiro kikali cha uchaguzi kinachokuja mwezi April kwa kuwafanya watu wasahau uchunguzi wa kashfa mbali mbali za ufisadi zinazomkabili.

(DW)