1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Rais wa China azuru Japan

Kalyango Siraj6 Mei 2008

Wachambuzi wanasema anajaribu kuondoa uhasama wa kihistoria kati ya nchi hizo mbili

https://p.dw.com/p/DuQe
Muandamanaji wa Kijapan akiwa na T-Shirt yenye maneno "Free Tibet" yenye maana 'Tibet Huru',akiwa na picha ya rais wa China Hu Jintao, ikiwa na maneno 'hakuna kuingia' wakati wa maandamano ya kupinga China mjini Tokyo May 6, 2008.Picha: AP

Rais wa China Hu Jintao ameanza ziara rasmi ya siku tano nchini Japan,ziara ambayo,wachambuzi wa mambo ya kisiasa wanaichukulia kama ya kuondoa uhasama wa mda mrefu wa mataifa mawili yenye uwezo mkubwa wa kiuchumi katika bara la Asia.

Ziara hii ni ya kihistoria ya aina yake kwa mataifa hayo mawili. Hii ndio mara ya kwanza kwa rais wa China kuzuru Japan baada ya mwongo mmoja na ya pili kuwahi kufanywa katika historia ya nchi hizo mbili.

Labda haya ndiyo matunda ya juhudi za miaka mingi za kumaliza sintofahamu ilioko kati ya mataifa hayo mawili yenye usemi mkubwa kiuchumi katika bara la Asia.

Rais Hu anatarajia kufanya mazungumzo na wenyeji wake kuhusu masuala mbalimbali.

Wachambuzi wa mambo wanasema mazungumzo yao yatajikita katika masuala kama vile halinya mazingira,mvutano uliopo ukihusu maeneo yenye utajiri wa gesi katika bahari ya East China Sea,sheria za usalama wa chakula cha China,shughuli za wakati wa vita vya Japan na China na huenda vilevile suala la Tibet.

Lakini tofauti na viongozi wa nchi za Ulaya ambao wanaonekana kuhepa sherehe za ufunguzi wa michezo ya olimpiki,Waziri mkuu wa Japan,Yasuo Fukuda,hata kabla ya rais Hu hajaafikiria ziara hii alikuwa ameamua kuwa yeye atahudhuria sherehe hizo.

Serikali ya Fukuda japo ilitoa maoni kuhusu Tibet na kukaribisha hatua ya serikali ya Bejing ya kufanya mazungumzo na wajumbe wa Dalai Lama,lakini wachambuzi wanasema ukosoaji wa Japan haukuwa wa makali sana.

Profesa mmoja wa Chuo kikuu cha Tokyo, Akira Ishii,anasema kuwa uhusiano kati ya nchi hizi mbili ni wenye utata sana kuliko uhusiano kati ya China na nchi za magharibi. Utata ni wa kihistoria.

China, wakati wa utawala wa waziri mkuu Junichiro Koizumi kati ya mwaka wa 2001 na 2006, ilikataa uhusiano wa ngazi za juu kutokana na kukasirishwa na hatua ya waziri mkuu wa wakati huo kutembelea kituo cha raia wa Japan waliopoteza maisha yao katika vita vya zamani miaka ya 40.Wakosoaji wanasema kuwa ziara katika kituo hicho ni kama kusifia uvamizi wa China ilioufanya dhidi ya mataifa mengi ya bara Asia miaka ya nyuma.

Lakini kwa sasa inaonekana China imeamua kupunguza matatizo yake na jirani zake wakati ikijaribu kuchukua mchango mkubwa zaidi katika medani ya dunia,kama vile na michezo ya Olimipiki.

Fukuda ametumia sehemu kubwa ya utawala wake kuridhiana na China

Maandamano ya kuunga mkono yalifanywa nchini humo wakati mwenge wa michezo ya Olipiki ulipofika Nagoya. Pia maandamano mengine yanapangwa kufanyika katika zaira ya rais wa China.

Japan ndio zaira ya kwanza ya rais Hu nje ya nchi tangu kutokea kwa maandamano makubwa mwezi Machi dhidi ya utawala wa China katika jimbo la Tibet.

Mkong'oto uliofuata maandamano hayo,umesababisha lawama kali katika jamii ya kimataifa na kuleta wasiwasi kuhusu michezo ya Olimipiki itakayofanyika Beijing kuanzia mwezi Agosti.