1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Rais wa Gabon awatuhumu waangalizi wa Umoja wa Ulaya

Admin.WagnerD7 Septemba 2016

Rais Bongo, ameijibu timu ya uangalizi ya Umoja wa Ulaya kwa kile ilichoeleza kumekuwa na ukiukwaji wa taratibu katika zoezi la kuhesabu kura baada ya uchaguzi wa Agosti 27.

https://p.dw.com/p/1JwzV
Gabon Wahlen Ali Bongo Ondimba
Rais wa Gabon Ali Bongo Ondimba wakati akipiga kura yakePicha: Reuters/G.W.Obangome

Rais Bongo ambae amekuwa madarakani tangu 2009, ameituhumu timu ya uangalizi ya Umoja wa Ulaya kwa kushiriki uangalizi unaokiuka taratibu na kuijiegemeza upande wa mpinzani wake Ping. Akizingatia matokeo katika eneo lenye wafuasi wake wengi la Haut-Ogooue amesema jana waangalizi walitao taarifa ya kutokea na makosa yoyote.

Kwa upande wao Umoja wa Afrika umesema utatuma ujumbe wake Gabon, ambao unatarajiwa kuongozwa na rais Idriss Deby, mmoja kati ya viongozi wa muda mrefu barani humo ambae pia ni mwenyekiti wa sasa wa Umoja wa Afrika. Ping ambae ni mwanadiplomasia na mwenyekiti wa Kamisheni ya Umoja wa Afrika wa zamani, anasema amepata taarifa kuwa ujumbe huo utawasili Alhamis.

Uchunguzi wa mchakato

Hatua ya kuchaguliwa tena, kwa rais Ali Bongo inakabiliwa na uchunguzi wa kimataifa baada ya jana Umoja wa Ulaya kuhoji uhalali wa ushindi wake finyu, Ufaransa ikipendeketza kuhesabiwa upya kura huku Umoja wa Afrika ukisema utatuma ujumbe wake nchini Gabon.

Gabun Libreville Ausschreitungen nach Wahlen
Taharuki ya wapiga kura baada ya uchaguzi mjini LibrevillePicha: Getty Images/AFP/M. Longari

Kiongozi wa upinzani Jean Ping, ambae anasema kulikuwa na wizi wa kura, alitoa wito kwa jumuiya ya kimataifa kuwasaidia watu a Gabon. Akizungumza na shirika la habari la Uingereza Reuters, kiongozi huyo alisema kila raia wa taifa hilo analifahamu hilo na kwamba Bongo anafanya kila linalowezekana kutokubaliana nalo.

Ping anasema idadai ya wapiga kura katika jimbo la kusini la Haut-Ogooue zimevurugwa na kumpa ushindi, rais Bongo ambae familia yake inaliongoza taifa hilo la Afrika ya kati, lenye kuzalisha mafuta kwa zaidi ya nusu karne. Takribani watu sita wameuwawa na wengie zaidi ya 800 wametiwa mbarini kufuatia vurugu zilizotokea kwenye mji mkuu, Libreville na maeneo mengine katika siku zilizofuata baada ya matokeo ya uchaguzi wa Agosti 27.

Uchaguzi huo ulimpa rais Bongo ushindi wa kura 5,000. Hata hivyo hali ya utulivu umerejea kidogo baada ya mitaa ya miji ya taifa hilo. Lakini mpinzani Ping amesema watu kati ya 50 hadi 100 wameuwawa mjini Libreville. Hata hivyo hakuna uthibitisho wa idadi hiyo ya watu.

Waangalizi wa uchaguzi walililenga jimbo la Haut-Ogoue, ngome ya Bongo, ambapo matokeo rasmi yanaonesha alishinda kwa asilimia 95.46 ya kura zote, idadi ya waliojitokeza ikiwa asilimia 99.9. Waangalizi wa Umoja wa Ulaya wa Ulaya wamesema idadi ya wasipiga kura ua zilizoharibika zilikuwa kinyume na taarifa, na kuongeza kuwa idadi ya waliojitikokeza katika mikoa mingine ilikuwa asilimia 48.

Gabon taifa lenye ukubwa unaofananisha na Uingereza lakini kuwa na idadi ya watu milioni 1.8, limewahi kuongizwa na marais watatu tangu kujiondoka katika mikono ya Ukoloni wa Ufaransa mwaka 1960.

Mwandishi: Sudi Mnette AFP/RTR
Mhariri:Yusuf Saumu