1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Rais wa Palestina Abbas kukutana na Ehud Olmert waziri mkuu wa Israel

20 Juni 2007

Baada ya kikao cha jana kati ya rais G.Bush wa Marekani huko Washington na waziri mkuu Olmert wa Israel,mkutano umepangwa kati ya rais wa Palestina na waziri mkuu wa Israel.Wapi na lini hasa utafanyika haifahamiki.

https://p.dw.com/p/CHCS
Wanachama wa Fatah wakimbia Gaza
Wanachama wa Fatah wakimbia GazaPicha: AP

Taarifa kutoka Ramallah,ukingo wa Magharibi, zasema kwamba rais Mahmud Abbas wa Mamlaka ya ndani ya wapalestina, atakutana na waziri mkuu Ehud Olmert wa Israel wiki ijayo mbele ya viongozi wa kiarabu na wa kimataifa.

Mjini Washington,rais G.Bush na waziri mkuu Olmert, waliahidi jana kumuimarisha rais Abbas na kuitenga kabisa Hamas huko mwambao wa Gaza ambako wanajeshi wa Israel waliwaua leo wapalestina 6.

Wanajeshi wa Israel wamewaua leo wapalestina 6 pamoja nao wane katika mwambao wa gaza ambako chama cha Hamas kinatawala.

Vifaru kadhaa na vikosi vilivuka mpaka na kuingia Gaza jana usiku –shahidi mmoja amearifu.Mwanajeshi mmoja wa Israel alijeruhiwa kidogo.

Katika Ukingo wa magharibi,vikosi vya Israel vimewaua wapalestina 2 katika mapigano yaliozuka karibu na mji wa Jenin.

Katika safu ya diplomasia kufuatia ziara ya waziri mkuu wa Israel huko Washington , rais Mahmud Abbas wa Palestina anaetawala ukingo wa magharibi pekee wakati Hamas ikudhibiti barabara mwabao wa Gaza, atakutana na waziri mkuu wa Israel Olmert wiki ijayo wakihudhuria kikao hicho viongozi wa kiarabu na wa kimataifa.

Yaser Abed Rabbo,mshirika wa chanda na pete wa rais Abbas, hakutaja ni lini na wapi mkutano huo utafanyika isipokua alisema maandalio yamo kufanywa.Ikifahamika hatahivyo, kwamba lile kundi la kimataifa la pande 4 linalohusika na mgogoro wa Mashariki ya kati –UM,Umoja wa ulaya, Marekani na Russia, lilipangwa kukutana Juni 26 na likitarajiwa kuwaalika tangu waziri mkuu Olmert hata rais Abbas.kumekuwapo taarifa lakini kuwa kikao hicho yamkini kikaahirishwa kutokana na msukosuko ulioibuka huko Gaza.

Jana rais Bush wa marekani na waziri mkuu Olmert wa Israel waliahidi kumtia moyo na kumpa nguvu rais Mahmud Abbas huku wakati huo huo wakiitenga kabisa Hamas inayokataa kuitambua Israel.Isitoshe, tangu rais Bush hata Olmert walithibitisha tena nia yao ya kuundwa dola la wapalestina lakini hawakutoa mpango madhubuti wa kuifikia shabaha hiyo.

Rais Mahmud Abbas, angependa kumuona rais Bush anaishinikiza Israel –mshirika wake wa chanda na pete-kuwaridhia wapalestina mambo kadhaa na kuanza mazungumzo ya amani ili aweze kuwaonesha watu wake wa Palestina aweza kupiga hatua kuelekea dola huru la Palestina.

Mjini Jeruselem,maafisa wa hadhi ya juu wa Israel na wa kambi ya magharibi wamesema kuwa Israel inapanga kuibana kabisa gaza kwa kuinyima msaada wote isipokuwa wa kibinadamu na wa mahitaji ya kimsingi ya kimaisha.

Waziri mpya wa ulinzi wa Israel, Ehud Barak, aliamuru jeshi la Israel kuwaruhusu idadi isio-tajwa ya wapalestina wanaoukimbia mwambao wa Gaza kuingia Israel na hasa kwa matibabu.Kiasi cha wapalestina 200 wamekwama mpakani mwa gaza na Israel.