1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Rais wa Ujerumani akamilisha ziara yake barani Afrika

Zainab Aziz
15 Desemba 2017

Rais wa Ujerumani Frank- Walter Steinmeir katika ziara yake barani Afrika alizingatia kuweka mfano sio tu katika suala la kupambana na uhamiaji haramu nchini Ujerumani bali pia kutafuta suluhisho kwa nchi hizo.

https://p.dw.com/p/2pQi0
Afrika Bundespräsident Steinmeier in Gambia
Picha: picture alliance/dpa/B. v. Jutrczenka

Rais wa Ujerumani katika  safari yake hiyo alitilia maanani masuala ya demokrasia na maendeleo ya kiuchumi lakini suala la uhamiaji pia liliendelea kujitokeza zaidi hasa nchini Gambia. Rais wa Gambia Adama Barrow akiwa yeye mwenyewe ni mmoja wa watu waliorudishwa nchini humo baada ya kuwa muhamiaji hapa nchini Ujerumani. 

Wakati Barrow alipokuwa na umri wa miaka 22, mnamo mwaka wa 1988, kwa kuvutiwa na hadithi za mafanikio kutoka kwa marafiki zake pamoja  na binamu zake hadithi hizo zilimvutia kuja barani Ulaya. Kama vijana wote, yeye pia aliamini kwamba nchini Ujerumani kuna fedha na baada ya kurejeshwa nyumbani amesema kuwa anaiona Gambia kama Ujerumani yake,Marekani yake,na vile vile kama Ulaya yake. Barrow aliyasema hayo wakati alipowahutubia vijana katika chuo cha mafunzo cha GTTI katika mji mkuu wa Banjul na kuongeza juu ya  madhila yaliyomkuta ya kurudishwa nchini mwake kutoka Ujerumani rais huyo alisema aliona kama dunia imemuangukia lakini juu ya yote hayo hakuteteleka katika imani yake.

Gambia Präsident Adama Barrow | Amtsübernahme & Einweihungszeremonie in Bakau
Picha: Reuters/T. Gouegnon

Rais huyo wa Gambia Adama Barrow alifanya kazi kwaa bidii katika kampuni yake ya  usalama ambayo aliianzisha kwa mtaji wa dola 1,200. Baada ya miaka 22 ya udikteta, Barrow aliongoza Mapinduzi ya Kidemokrasia kwa ushirikiano wa vyama saba. Na sasa amekuwa mfano bora wa mafanikio kwa vijana ambao wengi wao bado wana mawazo ya kuondoka nchini.

Mustafa Sallah amevutiwa na hotuba ambayo haikutarajiwa. Yeye pia amerejea nyumbani kama alivyofanya rais  Barrow.

Spanien | NGO "Proactiva Open Arms"
Picha: Getty Images/AFP/A. Messinis

Kijana huyo mwenye umri wa miaka26 mtaalam wa Tehama na msanifu wa michoro alifikiri kila chuo kikuu cha Ujerumani kingemchukua na kumpa udhamini lakini alikamatwa huko Tripoli kabla hata ya kuanza safari yake alizuiwa kwa wiki kadhaa jela, na huko aliweza kusikia hadithi za kutisha za vijana wengine. Mustafa amesema kama angelijua ukweli na mapema asingetaka hata kuondoka nyumbani. Kwa sasa Sallah anataka kufanya kila linalowezekana ili kuwazuia vijana wengine wasiingie kwenye njia hiyo ya hatari.

Wajumbe wa Ujerumani wana matarajio ya juu miongoni mwao wakiwa ni wafanya biashara wakubwa 18. Ushirikiano juu ya marekebisho ulifikiwa baina ya Ujerumani na Ghana nchi yenye  utajiri wa rasilimali. Wajasiriamali wengi wanaiona hatua hii kama misaada ya maendeleo ya kawaida wanakejeli kiasi cha Euro milioni 100 kama mikopo kwa ajili ya ununuzi wa mifumo ya nishati ya jua na iliyotengenezwa China wansema ni jambo la kushtua kwamba mpango wa kukuza uwekezaji hautoki kwenye makampuni ya Ujerumani wala ya Afrika, lakini kwa wajasiriamali wa Gambia wanaona kuwa hii ni fursa, hasa katika sekta ya nishati.

Mwandishi:Zainab Aziz/Claus Stäcker

Mhariri: Yusuf Saumu