1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Rais wa Ujerumani aonya kuhusu"kuwa na taswira ya adui"

Sekione Kitojo
24 Desemba 2016

Katika hotuba yake ya kila mwaka kwa sikukuu ya Krismasi, rais wa Ujerumani Joachim Gauck amesema hasira na chuki dhidi ya ugaidi isigeuke kuwa chuki

https://p.dw.com/p/2UpUr
Deutschland Weihnachtsansprache Bundespräsident Gauck
Rais wa Ujerumani Joachim Gauck Picha: picture-alliance/AP Photo/M. Schreiber

Hotuba  hiyo  ya  kawaida  ya  kila  wakati  wa  sikukuu  ya  Krismass  kutoka  kwa  rais  wa Ujerumani mwaka  huu  kwa  kiasi  kikubwa  ilihusika  zaidi  ya  tukio  la  Jumatatu  la shambulio   la  kigaidi  katika  soko  la  Krismass  mjini  Berlin. Watu 12 waliuwawa  na wengine  49  walijeruhiwa  baada  ya  anayedaiwa  kuwa  mshambuliaji Anis Amri kuendesha  lori  na  kuligonga  kundi  la  watu  Desemba  19.

"Vifo  vingi  na  majeruhi  katika  soko  la  krismass mjini  Berlin vimetuogopesha  na  kuwa kutukera," Rais Joachim gauck  alisema  katika  hotuba  iliyorekodiwa  kabla  na  kutangazwa kutoka  katika  kasri  lake  katika  mji  mkuu  la  Bellevue. "Watu wanajisikia  hasira , hofu  na kutokuwa  na  nguvu."

Berlin Virchow-Klinikum der Charite - Gauck besucht verletzte nach Anschlag
Rais wa Ujerumani Joachim Gauck alipowatembelea watu waliojeruhiwa mjini BerlinPicha: Reuters/C. Mang

Gauck  ameonya  kwamba  hisia  hizi hazipaswi  kuruhusiwa  kutawala,  na  kuongeza kwamba  hasira  haipaswi kugeuzwa  kuwa  chuki  na  ghasia. Badala  yake , ni  juu  ya  kuwa na  umoja  na  kulinda  hali  ya  kuishi  kwa  pamoja.

Mtu yeyote  ambaye  ana  hisia, yuko  tayari  na  mwenye  kusaidia" anaweza  "kubadili hasira  na  chuki  kuwa  nguvu  ambayo  inaweza  kuzuwia  chuki, ghasia  na  kuwatendea vibaya  wengine," Gauck  alisema  katika  hotuba  yake  ya  mwisho  ya  Krismass  akiwa rais  wa Ujerumani.

Mjadala  sahihi  wa  kisiasa

Gauck  alionesha  wasi  wasi  katika  uwezekano  wa  jamii  kuwa  na  msimamo  mkali - hususan  katika  mjadala  wa  kisiasa  kuhusiana  na  sera  ya  wakimbizi  nchini  Ujerumani. "Hususan  katika  wakati  wa  mashambulizi  ya  kigaidi, hatupaswi  kuongeza  kina  cha mipasuko  katika  jamii  yetu, ama  kuyashuku  makundi  ama  kuelekeza  vidole  kwa wanasiasa   nchini," Gauck  alisema.

Hii  haina  maana , hata  hivyo ,  kwamba  mijadala  ya  kisiasa  kuhusiana  na  sababu  na matokeo  ya  shambulizi  yanapaswa  kuachwa  kando; la  hasha, sera  za  wakimbizi  na usalama   nchini  Ujerumani  ni  lazima  vijadiliwe, lakini  kwa  kutumia  maamuzi  sahihi  na kuwasikiliza  wapinzani  wa  kisiasa. Kwa  Gauck , mchungaji  wa  zamani , hii  inahusiana sana  na  ujumbe  wa  kikristo  katika  krismass. "Hivi  sasa, katika  siku  kama  hizi, tunapaswa  kukumbuka  maana  ya   krismass   na  vipi  imekuwa  sehemu  ya  utamaduni wetu  kupindukia  Wakristo."

Deutschland Sicherheitsmaßnahmen Weihnachtmarkt am Breitscheidplatz
Polisi wakilinda soko la krismass mjini Berlin baada ya shambulioPicha: Reuters/H. Hanschke

Kuonesha  shukrani

Rais ametoa  wito  kwa  raia  wa  Ujerumani  kuwa  na  hali  ya  "kuiamini  nchini yao"  na kufanya  kila  linalowezekana  kuhakikisha  kwamba  jamii  inabakia "sehemu  ya umoja  wa mshikamano." "Hata katika  wakati  huu , wakati  nchi ikihangaika  na  masuala  ambayo hayajapatiwa  ufumbuzi, " Gauck  aliongeza. Hakuelezea "ndoto kubwa,"  lakini  alizungumzia badala  yake "kuhusu hali  halisi." Gauck  alisema  anaendelea  kukutana  na  watu  ambao wanaifanya Ujerumani  kuwa  mahali  pazuri  zaidi  pa  "kuishi" - iwapo  ni  kwa  kufanyakazi , starehe, katika  familia  ama  kwa  kujitolea. "Watu  hawa  mara  zote  wamenifanya niweze kujiamini  zadi  kama  rais," alisema.

Katika  hotuba  yake  ya  kila  mwaka  ya  Krismass, Gauck  pia  alitoa  sifa  maalum  na shukrani  kwa  wauguzi na  watoa  huduma,  waalimu wa  chekechea, waalimu, wanajeshi  na maafisa  wa  kisiasa. Lakini pia  kwa "vyama  vya  wafanyakazi  na  wafanyabiashara, wafanyakazi  wanaotoa  huduma  kwa  jamii na wanaohudumia   maeneo  mbali  mbali, na wote wanaofanya  sheria  inafanyakazi."

Shukrani  pia  zilitolewa  kwa "watu  wengi  wa  kujitolea  ambao  waliwasaidia  wakimbizi  na kuonesha  kwamba  hawapaswi  kuachwa  bila  ya  kuhudumiwa  na  kuwakataa  watu  kutoka nje  ili  kulinda  maisha  yao." Hususan  katika  nyakati  fulani, jamii  itakubali "kazi muhimu" za watu  hawa. " Sio kwasababu  wanafanya  kitu  ambacho  si  cha  kawaida," Gauck  alisema ," lakini  ni  kwa  sababu  wanafanya  vizuri  sana."

Mwandishi : Sabine Kinkartz / ZR /  Sekione  Kitojo
Mhariri: Zainab Aziz