1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Rais wa Ujerumani Joachim Gauck azuru Ufaransa

4 Septemba 2013

Rais wa Ujerumani Joachim Gauck yuko katika ziara ya siku tatu nchini Ufaransa. Leo (04.09.2013) atazuru magofu ya kijiji cha Oradour-sur-Glane pamoja na rais Francois Hollande wa Ufaransa.

https://p.dw.com/p/19bn4
Rais Gauck akiwa ParisPicha: Jacques Brinon/AFP/Getty Images

Rais Gauck wa Ujerumani, atahudhuria tukio la kumbukumbu katika kijiji hicho ambapo majeshi ya utawala wa Wanazi yaliwauwa watu 642 katika kijiji hicho Juni mwaka 1944.

Shambulio la gesi ya sumu nchini Syria amesema rais Gauck linahitaji kujibiwa kwa hatua kali. Alikuwa akizungumza katika mkutano na waandishi habari pamoja na rais Francois Hollande mjini Paris jana. Pamoja na hayo suala la Syria litajadiliwa baina ya nchi hizo mbili.

Bundespräsident Joachim Gauck spricht am 09.08.2013 in Lübeck vor dem Benefizkonzert des Bundespräsidenten im Rahmen des Schleswig-Holstein Musik Festivals auf der Bühne. Foto: Sven Hoppe/dpa +++(c) dpa - Bildfunk+++
Rais wa Ujerumani Joachim GauckPicha: picture-alliance/dpa

Kuishambulia Syria

Rais Gauck hakutaka kulijadili suala la kuchukua hatua anazozifikiria rais wa Ufaransa kuhusiana na shambulio la gesi ya sumu nchini Syria, lakini atasisitiza msimamo wa serikali kuhusu suala hilo.Rais Gauck amezungumza kwa simu na kansela kuhusu mzozo wa Syria. Kansela Angela Merkel anataka kwa mfano kulizungumza suala hilo katika mkutano wa kundi la mataifa tajiri na yale yanayoinukia kiuchumi ya G20.

"Hapa inahitajika kuchukuliwa hatua kali. Nimezungumza leo na rais na kumpa salam kutoka kwa kansela Angela Merkel, na ameniambia kuwa itakuwa busara suala hilo likazungumzwa katika mkutano ujao wa G20 na kufikiwa msimamo wa pamoja wa kimataifa kuhusu jibu sahihi katika mzozo wa Syria".

Gauck amesisitiza lakini, kuwa Ujerumani inachukua msimamo tofauti katika suala la kupeleka majeshi yake katika nchi za nje. Hatua hiyo ina msingi wa kihistoria na pia kisheria. Na serikali ya Ujerumani imekataa kushiriki katika hatua ya kuishambulia Syria katika siku za hivi karibuni.

France's President Francois Hollande reacts as he delivers a speech during the annual Conference of Ambassadors at the Elysee Palace in Paris August 27, 2013. President Hollande said on Tuesday that France stood ready to punish the perpetrators of a chemical attack in Damascus last week and would increase its military support to the Syrian opposition. REUTERS/Kenzo Tribouillard/Pool (FRANCE - Tags: POLITICS)
Rais wa Ufaransa Francois HollandePicha: REUTERS

Uamuzi wa Bunge

Kuhusiana na suala la iwapo bunge la Ufaransa litaamua leo kuhusu kuishambulia Syria , rais Hollande alijibu , na hapa ninamnukuu; " Hadi sasa bado hatujafanya hivyo." Badala yake bunge litajadili kile kinachofahamika hii leo kuhusu shambulio la gesi ya sumu. Rais Hollande amesema kuwa kunahitajika msimamo wa pamoja wa mataifa.

"Inategemea uamuzi wa bunge la Marekani, ndipo muungano utapatikana. Iwapo uamuzi wa bunge la Marekani hautaelekea kuchukua hatua, Ufaransa haitaweza kuchukua hatua pekee lakini italazimika kuwajibika".

Yalikuwa ni mauaji ya halaiki amesema Hollande, ni maafa katika wakati tulionao. Ushahidi tunao na mtu anayehusika anafahamika. Ni utawala wa Assad pekee uliopo katika nafasi ya udhibiti wa silaha za kemikali na ina teknolojia ya kuweza kutumia silaha hizo.

ATTENTION EDITORS - VISUALS COVERAGE OF SCENES OF DEATH AND INJURY Syrian activists inspect the bodies of people they say were killed by nerve gas in the Ghouta region, in the Duma neighbourhood of Damascus August 21, 2013. Syrian activists said at least 213 people, including women and children, were killed on Wednesday in a nerve gas attack by President Bashar al-Assad's forces on rebel-held districts of the Ghouta region east of Damascus. REUTERS/Bassam Khabieh (SYRIA - Tags: CONFLICT POLITICS CIVIL UNREST) TEMPLATE OUT
wahanga wa shambulio la gesi ya sumu SyriaPicha: Reuters

Kwa kuwa katika eneo lililoshambuliwa na gesi hiyo ya sumu kulikuwa na mawasiliano maalum ya kutumia gesi hiyo ya Sarin. Hollande ameonya inaweza shambulio kama hilo likafanyika tena.

Mkutano huo na waandishi habari umefanyika katika siku ya kwanza ya ziara ya siku tatu ya rais Gauck nchini Ufaransa . Marais hao wamesisitiza umuhimu wa ziara hiyo katika kumbukumbu ya miaka 50 ya mkataba wa urafiki baina ya mataifa hayo.

Mwandishi: Scholtz, Kay-Alexander / ZR / Sekione Kitojo
Mhariri: Iddi Ssessanga