1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Rais wa Urussi afanya ziara China

23 Mei 2008

-

https://p.dw.com/p/E4sb

BEIJING

Rais mpya wa Urussi Dmitry Midvedev leo anafanya ziara yake ya kwanza nje ya nchi tangu alipochaguliwa wadhifa huo ambapo anatembelea China.Rais Huyo atakuwa na mazungumzo na mwenzake wa China Hu Jintao pamoja na viongozi wengine juu ya masuala ya kibishara.Ushrikiano wa kibiashara kati ya nchi hizo mbili umepanuka kwa kasia katika kipindi cha miaka ya hivi karibuni.Ziara hiyo ya rais mpya wa Urussi imekuja wakati ambapo nchi zote mbili Urussi na China zimekosolewa na Marekani pamoja na nchi zingine za magharibi juu ya haki za binadamu na masuala mengine ya ndani . Medvedev anatazamiwa kutembelea Ujerumani mwezi Juni kukutana na kansela Angela Merkel ambaye mara kadhaa amekuwa akiikosoa Moscow.