1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Rais wa zamani Peru jela miaka sita

12 Desemba 2007
https://p.dw.com/p/Caf8

LIMA.Mahakama Kuu nchini Peru imemuhukumu kifungo cha miaka sita jela Rais wa zamani wa nchini Alberto Fujimori kwa kutumia vibaya madaraka yake.

Mahakama hiyo ilimkuta na hatia ya kutoa amri wakati wa utawala wake ya kupekuliwa kwa nyumba ya mke wa aliyekuwa mkuu wa ujasusi Vladimiro Montesinos November mwaka 2000.

Ni hukumu ya kwanza juu ya makosa ya kihalifu kwa kiongozi huyo wa zamani wa Peru ambaye pia anakabiliwa na mashtaka ya rushwa na ukiukaji wa haki za binaadamu.

Hukumu hiyo inaweza kuathiri utetezi wake katika kesi nyingine ya mauaji inayomkabili.

Fujimori aliitawala Peru kuanzia mwaka 1990 hadi mwaka 2000 alipokimbilia Japan baada ya serikali yake kuangushwa.