1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ramallah. Mapigano bado yanaendelea.

14 Mei 2007
https://p.dw.com/p/CC2G

Watu wawili wenye silaha katika eneo la mamlaka ya Palestina wameuwawa na wengine 11 wamejeruhiwa katika mapigano kati ya makundi hasimu ya Hamas na Fatah katika mji wa Gaza, licha ya makubaliano ya kusitisha mapigano yaliyokubalika usiku wa jana.

Duru za hospitali zimesema kuwa watu hao wawili waliouwawa ni wa chama cha Fatah.

Mapigano yalizuka saa chache baada ya maafisa kutoka kila upande kutangaza makubaliano ya kusitisha mapigano , baada ya Wapalestina wanne kuuwawa katika mapigano ya kimakundi wishoni mwa juma.

Mwezi wa March Hamas na fatah walijiunga pamoja kuunda serikali ya umoja wa kitaifa kwa lengo la kumaliza mapigano hayo kati ya makundi hayo mawili hasimu.