1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

RAMALLAH: Wakimbizi wa Kipalestina kurejea nyumbani

28 Julai 2007
https://p.dw.com/p/CBeP

Kiasi ya wakimbizi 6,000 wa Kipalestina wanaweza kurejea makwao kutoka Misri,baada ya kuwa na dhiki ya majuma kadhaa.Serikali za Israel na Misri zimekubaliana kuwaruhusu Wapalestina hao kurejea nyumbani.Wakimbizi wa mwanzo,wataruhusiwa kupitia mpakani mwa Israel,siku ya Jumanne. Kutoka hapo,maafisa wa Kipalestina watakuwa na dhamana ya kuwasafirisha wakimbizi hao katika mabasi,hadi Ukanda wa Gaza.Baada ya chama cha Hamas chenye sera kali za Kiislamu,kudhibiti Ukanda wa Gaza kama majuma sita yaliyopita,maelfu ya Wapalestina wamenasa katika miji ya Misri,kaskazini mwa eneo la Sinai.