1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

RAMALLAH: Wapalestina wajaribu kuunda serikali ya umoja wa taifa

12 Novemba 2006
https://p.dw.com/p/CCtP

Makundi makuu mawili ya Wapalestina,yanakutana kwa mazungumzo ya kuunda serikali ya umoja, yakiwepo matumaini kuwa baraza jipya la mawaziri litakubaliwa baada ya mvutano wa miezi mitano. Majadiliano kati ya chama cha Fatah cha rais Mahmoud Abbas na chama tawala cha Hamas yatamakinikia muundo na mfumo wa serikali.Kwa miezi kadhaa,rais Abbas alikuwa akizozana na chama cha Hamas kuhusu suala la kuunda baraza la mawaziri la umoja,kwa azma ya kupunguza matatizo ya kisiasa na kifedha yanayokabiliwa na maeneo ya Kipalestina kwa kiwango ambacho hakijawahi kushuhudiwa.Chama cha Hamas,kimengángania msimamo wake wa kutotekeleza madai ya nchi za magharibi kuitambua Israel.Siku ya Jumamosi,Abbas alisema anatazamia kuona serikali ya umoja ikiundwa kabla mwisho wa mwezi Novemba.