1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ramallah:Ban Ki-moon aizuru kambi ya Wapalestina ukingo wa magharibi

25 Machi 2007
https://p.dw.com/p/CCFP

Katibu mkuu wa Umoja wa mataifa Ban Ki-moon,ameitembelea kambi ya wakimbizi wa kipalestina katika ziara yake ya kwanza katika ukingo wa magharibi, tangu ashike wadhifa huo miezi miwili iliopita. Mkuu huyo wa umoja wa mataifa pia aliukagua uzio uliojengwa na Israel katika mpaka na ukingo wa magharibi jambo ambalo limesababisha malalamiko makali. Bw Ban alisema atautaka uongozi wa Israel usitishe utanuzi wa makaazi na ujenzi wa uzio huo. Kabla ya kuonana na Rais Mahmoud Abbas, katibu mkuu wa umoja wa mataifa alilizuru kaburi la mtangulizi wa Abbas, hayati Yasser Arafat. Bw Ban amekataa kuonana na Waziri mkuu Ismail Haniya kutoka chama cha Hamas, kwa sababu bado kinakataa kulaani matumizi ya nguvu na kutambua haki ya kuishi dola ya Israel.