1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Rangoon. Amri ya kutotembea usiku yaondolewa.

21 Oktoba 2007
https://p.dw.com/p/C7E1

Utawala wa kidikteta nchini Burma umeondoa amri ya kutotembea usiku katika mji mkuu wa nchi hiyo Rangoon, amri ambayo iliwekwa mwezi uliopita baada ya maandamano makubwa kuipinga serikali.

Tangazo hilo , lililotolewa kupitia gari lililokuwa limewekwa vipaza sauti lililopita katika mitaa ya mji huo pia limemaliza marufuku dhidi ya mikusanyiko ya zaidi ya watu watano. Haikufahamika iwapo amri kama hiyo katika mji ulioko katikati ya nchi hiyo wa Mandalay, ambao pia ulishuhudia maandamano dhidi ya utawala huo wa kijeshi, kama imeondolewa.

Amri ya kutotembea usiku iliwekwa Septemba 25, wakati jeshi lilipoanza kuzima maandamano ya amani yaliyokuwa yakifanywa na watawa wa Kibudha dhidi ya miaka 45 ya utawala wa kijeshi nchini humo.